ASILI YA CHRISTMAS.
Mwanzo
10:8
Katika
kitabu cha Mwanzo 10:8 tunakuta habari za mtu mmoja maarufu kwa jina anaitwa
Nimrod alikuwa mtu maarufu sana katika zama zake. Tena alikua mfalme wa kwanza
wa kibinadamu katika Biblia. Nimrod ananenwa kuwa mtu hodari, katika Mwanzo
10:8-12, mwanzo wa ufalme wake ni babeli; Ereku, Akadi, Kalne, Ashuru, akajenga
ninawi na Rehobothiri, Kala na kati ya ninawi na Kalanago ilikuwa ni miji
mikubwa. Mke wa Nimrod aliitwa Shemiramis.
SIFA ZA NIMROD (NIMRUDI).
A. Mwenye
hekima nyingi.
B. Mwenye
kipaji cha kutawala .
C. Mwenye
ujuzi wa mambo.
D. Mwenye
uwezo na nguvu za kushawishi.
E. Mwenye
mawazo makubwa.
F. Mwenye
uwezo wa kutenda.
G. Mawazo
yake yalikubaklika na watu wote.
H. Ndiye
aliyejenga mji wa Ninawi na mji wa
Babeli.
I. Alijenga
ukuta wa Babeli kuzungukia mji wote ili
kuweza kukomesha tatizo la wanyamapori wakali waliokuwa wakiwasumbua.
J. Alishawishi
watu wajipatie mfalme atakayewaongoza mara baada ya kumaliza kujenga ukuta, na
kutokana na uhodari na umaarufu wake wa kudhibiti wanyamapori wakali aliteuliwa
na kufanywa kuwa mfalme wa kwanza aliyetajwa na Biblia kwa wanadamu.
K. Alikuwa
ni mfalme asiyemcha Mungu.
L. Alikuwa
ni kuhani wa ibada ya shetani (miungu) na mpagani wa kutisha.
M. Nimrod
kuhai mfalme alikufa.
N. Kutokana
na umaarufu wake na kwa vile alikuwa mfalme wa kwanza wa taifa hilo, wanadamu
waliomboleza sana juu ya kifo chake huko Babeli alikotawala, lakini cha ajabu
hata baada ya kifo chake dini ya babeli aliyoianzisha iliendelea hadi leo.
Baada
ya miaka ya kifo cha Nimrod, malkia alizini na kuhani wake wa Matambiko katika
ibada ya jua. Katika kuzini na kuhani huyo malkia alibeba mimba, kwakuwa
alikuwa malkia na hana mume, na huku ana-mimba , watu wake walimuuliza kwamba
hii mimba imetoka wapi (ni yanani?) huku huna mume?
Kwa
makini na utaratibu malkia alijibu kwamba nilipokua nimeamka asubuhi nilitoka
kwenda kuota jua, mionzi ya jua ilinipiga tumboni nikasikia dalili za mimba na
mimba ikaanza kukuwa taratibu, shemiramis asingesema uongo huo angeuawa na watu
wake kutokana na mila na desturi za watu hawa. Shemiramis alibeba mimba tarehe
25/3…alijifunguwa tarehe 24 kuamkia tarehe 25/12…
SHEREHE YA KUZALIWA KWA
TAMMUZ.
Katika
asubuhi ya tarehe 25/12…ilikuwa ni sherehe kubwa sana ya kuzaliwa kwa mtoto TAMMUZ, pia iliaminika kwamba huyu mtoto
ni mtakakatifu, kwakuwa mimba yake imetokana na mionzi ya jua, pia iliaminika
kwamba Nimrod aliendelea kuzaa na mke wake huku akiwa katika jua. Yeremia 7:17-18
inaonyesha sherehe aliyofanyiwa katika kuzaliwa kwake (TAMMUZ), Sherehe hiyo iliridhiwa na wana wa Israel. Wakina baba na
akina Mama na watoto wote walijumuika katika maandalizi ya sherehe hiyo kubwa.
Yeremia 7:18, yeremia 52:31.
KIFO CHA TAMMUZ.
Hata
hivyo mtoto huyu alifariki dunia baada ya kipindi cha miaka mitatu tu.
Maombolezo makubwa yalifanyika ili kumuombolezea TAMMUZ. Wazee, wakina mama na watoto wote,
waliomboleza kwa machungu sana(Ezekieli 8:14). Shemiramis mke wa Mfalme Nimrod
akazua uongo mwingine, kwamba alienda kwa mungu hera, mungu hera alimpa
masharti kwamba awakusanye wanawake wote wafunge kwa siku arobaini(40) ndipo
ombi lake litafanikiwa. Shemiramis akafanya hivyo akawakusanya wanawake wote na
kufunga nao siku 40. Huu ndiyo mwanzo wa kwarezma.
MTI WA
CHRISMAS(MKRISMAS) NA IBADA YA UMIZIMU.
Katika
mashariki ya kati, Neno “T”, ni ishara ya takatifu. Kwani ulikuwa ni mti
waliokuwa wakitolea kafara. Maana ya Tammuz ni mungu katika mwili(T-mungu
mwili). Walipokuwa wakitoa kafara katika mti huu, uliitwa X-MASS.
Ø X =
hakuna,
Ø Mass
= sherehe.
Ø X + MASS = Hakuna
sherehe yoyote.
Mti
huo ulioitwa x-mass waliokuwa wakitumia kufanya kafara zao ambapo x-mass
ilionyesha hakuna sherehe katika eneo hilo la kufanyia kafara. Watu wote
walikaa kimya katika ibada hii ya Miungu. Mti huo leo unaitwa mkrismas(Mti wa
chrismas). Lakini pia Makuhani waliokuwa wakihudumu katika ibada hizo za miungu
walikuwa wakivaa alama ya “T” shingoni au kwente bega kuonyesha utakatifu. Shetani
alifanya mpango, mwana wa Mungu naye akatolewa kafara kwenye mti huu wa LAANA
ambao ni ishara takatifu ya shetani Galatia 3:13.
MIUNGU MIKUU:
Katika
makabila ya mashariki ya kati wana miungu yao mikuu ambayo ni; jua, mwezi na
nyota kati ya miungu yote, katika miungu hii, Nimrod kuishi kwenye jua, Shemiramis
kuishi kwenye Mwezi na motto(Tammuz) kuishi kwenye Nyota 2wafalme23:5. Mambo
hayo waisrael walirithi kutoka Babeli, na kuyafanya, warumi pia wameyarith na
kuyazingatia kwa kuyarekebisha. Lengo la shetani kufanya mfano huu wa Utatu
mtakatifu; yaani wakaufananisha utatu mtakatifu wa mbinguni na miungu yao kama
ifuatavyo;
v MUNGU
BABA = mungu jua = Nimrod.
v MUNGU
MWANA = mungu mwezi =Shemiramis.
v MUNGU
ROHO MTAKATIFU = mungu nyota = Tammuz.
CHRISTMAS (KRISMAS).
Kuzaliwa
kwa Tammuz, tarehe 24 kuamkia 25 mwezi wa 12 kuliambatana na sherehe iliyofanyika
kwa kuzaliwa kwa mtoto Tammuz, Yeremia 7:17- Leo imegeuzwa kuwa ni siku ya
kusherehekea kuzaliwa kwa YESU Kristo Mwana wa MUNGU jambo ambalo siyo sahihi.
Kilicho badilika hapa ni badala ya kutumia jina la Tammuz wamebandika jina la
YESU huku wakiendelea na matendo yao maovu hasa katika siku hiyo.
KUFUNGULIWA WAFUNGWA + KUZALIWA KWA
TAMUZI = KUZALIWA KWA YESU?
Katika
tarehe 25/12 ilikuwa siku ya
kusherekea kuzaliwa kwa Tammuz.
Kwa leo wanasherekea kuzaliwa kwa Yesu
ambapo si kweli, ni mpango wa kuendeleza
utukufu wa miungu ile ya zamani. Sikukuu nyingi na sherehe nyingi za kimataifa
katika nchi za mashariki huwa zinafanywa kwa kufuata siku maalum zinazotumika
katika kuheshimu miungu yao. Kwa mfano 25/12 kila mwaka hutumika kwa
kuwaachia baadhi ya wafungwa kuwa huru,
na tangu zamani hata katika taifa la Mungu. Chukulia Tanzania kwa mfano, kila
mwisho wa mwaka Rais anatoa msamaha kwa
baaadhi ya wafungwa, ni utamaduni uliorithiwa
tangu huko zamani lakini pia kusherekea kuzaliwa kwa mtoto Tammuz
,ambapo leo anasingiziwa Yesu.
MAAJABU
YA SIKU ZA SIKUKUU
Katika
siku hizi zote kristmas, pasaka kuna mambo makubwa yanayotendeka siku hiyo, hata kushangza viongozi wanchi
mbalimbali. Hata wakuu wa dini
hubaki kushangaa, ijapo wenyewe ndio
viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali yanayohusika kusimamia, kutetea
na kushawishi kushiriki katika sikukuu
hizo. Sikukuu ya Pasaka, Kristimasi na
Ramadhani na Siku ya Wapendanao. Badala ya kuabudu huyo Mungu wa mbinguni siku
hizo zimekuwa zikitumika kuongeza maambukizi ya
magonjwa ya zinaa ukiwemo ugonjwa
wa UKIMWI, kwani watu wengi siku hiyo huzini bila huruma, watu wanaosherekea
kwa kuzini na wanawake na wanaume. Ndoa nyingi huwa kwenye mgogoro.
Siku hiyo watu hunywa pombe na kulewa ovyo ovyo, wakiyatoa matusi mengi na mazito toka midomoni mwao, ugonvi, kubomoa nyumba na
vibanda vya watu, kupanga mawe njiani,
kuchoma Tairi za magari barabarani, watu kuendesha magari ovyo na kwa fujo
wakisababisha ajali nyingi na hata za makusudi. Watu wanalewa mpaka wanalala
uchi mitaani, “kama unataka kuona uchi wa mkwe wako tegea siku hiyo ya
kusherekea akilewa hatajitambua, atajikojolea
ovyo, kulala uchi basi nawewe katika kumsaidia ili asiaibike zaidi utakuwa
umemuona” . Askari katika dunia nzima hawapumziki nao waifurahie hiyo sherehe
bali hukaa chonjo wakipambana na wahalifu wanaozidi na kuongezeka siku hiyo.
Siku hizo ni siku za ANASA, Wanyama na ndege wanakuwa na maombolezo makuu kwani
si Mbuzi, Ng`ombe, Kuku na wengineo wanaoliwa, huchinjwa bila huruma eti kwa kuwa Mwanadamu anasherekea.
MAADIKO MATAKATIFU YANASEMA
NINI KUHUSU SIKUKUU HIZI:
Mungu
hapendezwi na sikukuu hizi hata kidogo, kwani kama zingekuwa na utukufu ndani
yake yasingefanyika machafuko na maovu haya
yote. Mungu atakomesha furaha zao na sikukuu zao,(Hosea
2:11, Isaya 24:7-10, Amosi 5:5). Mungu hapendezwi na sikukuu hizi kwani ni
kufuru kwake na hakuna fungu lolote katika biblia linalosema kuwa Yesu alizaliwa tarehe ngapi,
na wala katika siku za sikukuu hizi, tuliyofunuliwa na mungu ni yetu na watoto
wetu, tusiyofunuliwa hayo ni ya Mungu mwenyewe( tutayafahamu tukifika mbinguni,
tutamuuliza Baba habari za mambo hayo tusiyoyajua).
Utaratibu
wa sikukuu hizi ni mpango wa shetani kuendelea kuabudiwa na kuabudu miungu kwa
kujua au kutojua kwa kutumia pazia lenye jina jingine ili kificha ukweli lakini
kiini cha maovu na kufuru kwa Mungu Baba zikiwa zinaendelea kwa kasi siku hizo.
MAMBO UFANYAYO
KUSHIRIKI SIKUKUU HIZO BILA KUJUA AU KWA KUJUA.
1) Kutuma
ujumbe kwa simu, kadi na barua au zawadi maalum ya kumpongeza au kumtakia
sikukuu njema. Hii inamaana unakubaliana naye juu ya hicho anachotaka kukifanya
nawe unamuunga mkono na kumtia moyo asonge mbele.
2) Kuingia
gharama ya kununua mavazi ya kuvaa siku hiyo ya sikukuu. Kama huna mpango wa
kusherekea, kwanini unataka ufanane na wenye mtazamo huo wa kuonekana wapya kwa
hadhi ya siku hiyo?
3) Kutumia
siku hiyo kuma siku yako ya kutalii na kutemelea sehemu mbalimbali ambazo ni
rahisi kukuondoa katika mtazamo wa kiroho.
4) Kuhudhuria
mialiko mbalimbali uliyoalikwa kwa siku hiyo.
MAJINA
TOFAUTI YA TAMUZI
Maana ya jina Tamuzi ni mungu mwili kama tulivyokwishaona, lilikuwa
ni jina la kikabila. Lakini hatahivy
Tamuzi alijulikana kwa majina mbalimbali katika sehemu tofauti tofauti.
I.
Kisumeri maana ya jina
lake ni DUMUZI (mungu wa mavuno na mazao).
II.
Kikaanani alijulikana
kama BAALI.
III.
Kiefeso lilimaanisha ARTEMI.
IV.
Asia, lilimaanisha ASHTORETH.
V.
Kilatini lilimaanisha
ISHTAR.
VI.
Kiingereza lilijulikana
kama EASTER na
VII.
Kiswhahili
lilimaaanisha PASAKA.
MTIRIRIKO WA DOLA ZILIZOMWABUDU TAMMUZ
Tammuz aliabudiwa katika dola zifuatazo:
A. Dola
ya Babeli mwaka 605 B.C hadi 538 B.C.
B. Waamedi
mwaka 538 B.C hadi 331B.C .
C. Wayunani
mwaka 331 B.C hadi 168 B.C na
D. Warumi
mwaka 168 hadi 478 A.D
N.B;
Tammuz aliendelea kuabudiwa kwa namna ambayo ilianzishwa na mfalme wa Rumi
ya kipagani `Constatino mwaka wa
312 A.D` kama ifuatavyo;
1) Aliidhinisha
ibada ya maadhimishonya siku ya jua, Sunday (Jumapili) siku ya kuabudu jua
badala ya Sabato (Sturday) siku ya BWANA ambayo ni siku ya saba ya juma
(Alibadili sabato ya jumamosi).
2) Mfalme
Constantine pia aliadhimisha siku ya tarehe 25/12 kuwa siku maalumu kwa
kuzaliwa Mtoto Yesu, kwa ukweli Mtoto Tammuz alizaliwa tarehe 25 December na
kuzaliwa kwake kunaadhimishwa na Ukristo wa leo kama kuzaliwa kwa Yesu. Tarehe 25
ya mwezi wa 12 ilisherehekewa kumkumbuka Mtoto Tammuz katika dola ya Babeli,
katika siku hii wafungwa waliofungwa gerezani walifunguliwa na kuwekwa huru.
Soma Yeremia 52:31-34.
3) Sikukuu
ya EASTER ambayo inafanyika mwishoni mwa mwezi wa Tatu (March) au mwanzoni mwa
mwezi wa Nne (April) ni idhinisho la Tatu lililosimikwa na Mfalme Constantine.
Wakristo wanadai kumba ni ibada ya kukumbuka kufa kwa Bwana Yesu. Historia
ikowazi katika jambo hili kwamba ni katika kipindi hiki cha EASTER ambapo
wapagani walikuwa wanaomboleza kwa kufa kwa Mtoto Tammuz aliyezaliwa tarehe 25
December na kuaminiwa kupatwa na mauti mnamo mwishoni mwa mwezi wa tatu au
mwanzoni mwa mwezi wan ne. kwa sasa ni ukumbusho wa kifo cha Yesu na sio
Tammuz.(Oxford Dictionary-Constantine History).
4)
Vilevile katika karne
ya nne Mfalme Constantine aliadhimisha ibada ya kumuabudu Mama yake Yesu (Bikra
Maria) ambaye kwa sura zijazo tutaona jinsi ambavyo Malkia Shemiramis au mke wa
Nimrodi aliyepewa jina la Mariamu Mama yake Yesu ili kuingiza upagani katika Ukristo.
MWISHO.
Miongoni
mwa sikukuu zilizotajwa hapo juu (krismas,pasaka,ramadhani na siku ya
wapendanao), Hakuna hata moja inatoungwa mkono na MAANDIKO MATAKATIFU endapo
mtu ataamuwa kushiriki kwa namna yeyote ile ni kwa ukaidi wake mwenyewe. Mambo
hayo hayaungwi mkono na maandiko matakatifu wala vitabu vya ROHO YA UNABII.
Mambo yanayotendeka ni makufuru kwa Mungu wa Mbinguni.
Somo
hili ni sehemu ya kwanza, sehemu ya pili itahusu;
(i)
Mwanzo wa Ibada ya Mama
na Mtoto.
(ii)
Mwanzo wa Ibada yenye
matumizi ya Rozali(shanga).
(iii)
Mwanzo wa siku ya
wapendanao.
(iv)
Mwanzo wa sikukuu ya
Ramadhani.
(v)
Father Santa Clause ni
nani?
Bila shaka sasa
kila mmoja wetu amegundua ukweli kwamba
krismasi ni sherehe ya kipagani na
kwa hivyo anawajibu wa kubadilisha mtazamo wake na kujikita katika maandiko ili kuendelea kuujua ukweli na kuepuka kudanganywa .
Compiled
By Mogenge Emmanuel.