Thursday, 20 December 2012

UZOEFU WA WOKOVU...1




MFULULIZO WA MASOMO YA MISINGI YA IMANI YA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO.

10: MSINGI WA KUMI - UZOEFU WA WOKOVU.

            Uzoefu wa wokovu ni safari ya maisha ya mwenye dhambi akipitia hatua au njia mbalimbali mpaka afikie wokovu. Njia hizo ni; kuamini, kutubu, kuungama, kusamehewa, kuhesabiwa haki na kutakaswa.
FUNGU KUU: “ kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani;ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha MUNGU” Waefeso 2:8.
  1. Neema ni nini? Waefeso 2:8
Maelezo: Neema-Ni “huruma na upendo tele wa Mungu unaookoa wenye dhambi wasiostahili kuupata kama ulivyofunuliwa katika kristo. Ni upendo unaobadilisha, usio na mipaka na unaohusisha wenye dhambi wajinsi zote. Neema hii siyo tu huruma ya Mungu inayomfanya akubali kumsamehe mwenye dhambi, bali in nguvu ya kuokoa”. Kwa maneno mengine NEEMA ni huruma, wema na fadhili ya Mungu kwa binadamu asiye stahili kuokolewa.
  1. Imani ni nini? Waebrania 11:1
Maelezo: Imani ni sifa na hali ya kumtumaini Mungu kwa kuamini kwamba anatupenda na anajua zaidi kile kilicho na faida kwetu. “Imani ni kuwa na hakika ya mambo yasiyoonekana na ni bayana ya mambo yatarajiwayo”.
  1. Imani inayoleta wokovu ni ipi? Yahana 3:16
Maelezo: kwavile zipo imani za aina nyingi sana, wanatheologia wanaitafasiri imani inayoleta wokovu kama “imani iletayo wokovu siyo ile yakuwezesha kukubali ukweli tu, ni imani inayompokea kristo kama mokozi binafsi ikiwa na uhakika kwamba YESU anaweza kuwaokoa wote wanaokuja kwa Mungu kupitia kwake. Mtu anapomtegemea YESU kama tumaini lake pekee la wokovu basi hapo imani ya kweli imejifunua”.
  1. Ni kwanjia gani tunapata imani? Warumi 10:17,9-10.
“Imani huja kwa njia ya kusikia, na kusikia huja kwa njia ya neno la Mungu.” “Ikiwa utakiri kwa kinywa chako, kuwa YESU ni Bwana na kuamini kwamba Mungu alimfufua toka katika wafu utaokolewa. Kwakuwa ni kwa moyo wako unaamini na kuthibitika, na nikwakinywa chako  unakili basi utaokolewa.”
  1. Imani na injili: Ili mtu aokolewe sharti afanye nini? Warumi 1:16.
“kwakuwa siionei haya injili, kwasababu ni uweza wa Mungu uletao wokovu, kwa myahudi kwanza na kwa myunani pia.”

B: KUTUBU.
           
FUNGU KUU: 1Yhana 1:9
“Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wahaki hata atusamehe makosa yetu na kutusafisha na udhalimu wetu wote.”
1.      Je, kutubu ni lazima katika mpango wa wokovu? Matendo 17:30
Maelezo: “kutubu ndiyo hatua ya kwanza ambayo ni lazima kuchukuliwa na wote ambao wanataka kumrudia Mungu. Inatupasa kila mtu anyenyekeze moyo wake mbele za Mungu na kuacha nia yake mbaya.
2.      Mtu anaweza kufanya nini ili dhambi zake zisafishwe? Matendo 3:19
Maelezo: Maranyingi tunahuzunika kwasababu matendo yetu maovu yanatuletea matokeo mabaya kwetu sisi wenyewe, lakini hii sio toba. Huzuni halisi ya dhambi ni matokeo ya kazi ya Roho Mtakatifu. Kila dhambi humtonesha YESU vidonda vyake, na tunapo mtazama YESU, ambaye sisi tuliomuumiza tunaomboleza kwa sababu ya dhambi zilizomletea maumivu. Maombolezo hayo yanatuongoza kuacha dhambi.
3.      Wenye dhambi wanaongozwaje kwenye kutubu? Warumi 2:14" Kwa maana watu wa mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe." hivyo kuna nguvu isiyo ya kawaida inayokusukuma kutenda kwa namna ya sheria japo huijui sheria yenyewe. mfano mtu asiye na sheria ya Mungu hawezi pia kumuoa au kuolewa na Mama au Baba yake, kwa tabia hiyo imekuwa sheria kwake. je, ametambuaje kufanya hivyo kuwa si vyema?
4.      Jambo gani  linalofuata ungamo la kweli? Mithali 28:13
Maelezo: Ungamo haliwezi kukubaliwa na Mungu pasipo toba na matengenezo ya dhati. Nilazima pawepo mabadiliko ya lazima katika maisha, na kila kinacho muudhi Mungu lazima kiachwe kabisa. Jambo hili litakuwa na matokeo ya huzuni halisi ya dhambi.
5.      Kuungama kungalifanywa kwa nani? Zaburi 32:5
Maelezo: Ungameni dhambi zenu kwa Mungu ambaye yeye tu ndiye awezaye kuzisamehe. Namakosa mliyokoseana nyinyi kwa nyinyi ungamanianeni nyinyi kwa nyinyi ili Baba yenu wa mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.
            Ukimkosea ndugu yako au jirani yako itakubidi kulikubali kosa lako na niwajibu wake kukusamehe bure. Ndipo unapaswa kuomba msamaha kwa Mungu wa Mbinguni, kwasababu huyo nduguyo uliyemkosea na kumuumiza ni mali ya Mungu. Na kwa kumuumiza ulimtenda dhambi Muumbaji na Mokozi wake.
6.      Kuna ahadi gani juu ya dhambi ambazo zimeungamwa? Ebrania 8:12, ".....nitawasamehe maovu yao, na dhambi zao sitazikumbuka tena."
7.      Mtu ambaye amesamehewa dhambi zake anakuwa na hali gain? Zaburi 32:1,2
"Heri aliyesamehewa dhambi, Na kusitiriwa makosa yake. Heri BWANA asiyemhesabia upotovu, Ambaye rohoni mwake hamna hila." ukisamehewa dhambi zako utakuwa na amani moyoni kwani hutakuwa na hatia inayokusuta rohoni mwako.
8.      Kusamehewa kwetu na Mungu kunategemea vipi uhusiano kati yetu na wengine? Marko 11:25 - 26
" Nanyi, kilamsimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe na ninyi makosa yenu. Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu."  Mathayo 6:14,15. Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu."
9.      Je, Mungu atakumbuka dhambi zetu baada ya kutusamehe? Yeremia 31:34.
"........asema BWANA; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena." Ebrania 8:12, Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena."
10.  Je,Mungu atasamehe dhambi kiasi gain? Isaya 1:18
" Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu."

MWISHO:

1 comment:

  1. This scriptures should be considered to be more spiritual than social.

    ReplyDelete