TANZANIA HIGHER LEARNING
INSTITUTIONS OF
SEVENTH DAY
ADVENTIST STUDENTS ORGANIZATION(THISDASO).
“FUNGUA MASIKIO” Mithali 28:9
SOMO la 1.
MAWASILIANO.
Mawasiliano ni njia inayotumiwa na
watu au viumbe hai vingine kupeana habari, mawazo au hisia mfano; mavazi,
kuimba, machozi n.k
Mawasiliano ni neno pana na lenye
kubeba mambo mengi mbalimbali katika nyanja tofautitofauti.
Mawasiliano katika maisha ya binadamu
ni ya muhimu katika nyanja zote kiroho, kimwili, na kiakili.
MAWASILIANO NA MUUMBAJI WETU.
·
Sisi
kama vijana wa kiadventista, washiriki, wasomi na watu wote tunapaswa kujenga
mawasiliano mazuri na Muumbaji wetu kwa kumtambua yeye ni nani? Na umuhimu wake
ni upi kwetu.
Mfano: tunapaswa kuwa watu wa maombi ili uhusiano wetu uwe karibu na muumbaji wetu.
Wafilipi 4:6, Luka 18:1
Wafilipi 4:6 “Msijisumbue kwa neno lolote, bali kwa kusali
na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
Luka 18:1 “Akawaambia
mfano ya kwamba, imewapasa kumuomba Mungu siku zote wala wasikate tamaa.
·
Kupitia
mawasiliano, tunaaswa kumtukuza Muumbaji wetu na kumheshimu kupitia muonekano
wetu, mavazi, usemu wetu, ulaji na mitindo yote ya maisha. Ili vijana wenzetu,
watu wanaotuzunguka wapate kumuona Yesu na kujifunza kupitia kwetu.
1 Wakorintho 15:33 “Msidanganyike mazungumzo mabaya huharibu
tabia njema”.
1 Wakorintho 10:31 “Basi mlapo, au mnywapo, au mtendapo. neno
lolote fanyeni yote kwa ufukufu wa mungu.
MAWASILIANO NA WATU WANAOTUZUNGUKA.
·
Tunapaswa
kuwa na mahusiano mazuri na watu wote bila kujali matabaka yaliyopo, elimu na
kuona watu wote ni sawa na kumuona mwenzako ni bora kuliko wewe,ili iwe rahisi
kuwapatia ujumbe wa HABARI NJEMA YA UPENDO WA MUNGU na tumaini la kurudi kwa
Yesu mara ya pili kama utume wetu tulioitiwa.
Mathayo 28:19- “ Basi enendeni mkawafanye mataifa yote”kuwa
wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba,Mwana na Roho mtakatifu”
Wafilipi 2:3 “Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno,
bali kwa unyenyekevu,kila mtu na amhesabu mwenziwe bora kuliko nafsi yake”
·Kupitia
mawasiliano,tunapaswa kuwakilisha msimamo wa imani yetu
ya kudumu kuwa washiriki waaminifu katika usemi,mwenendo,usafi na imani ili
watu wajifunze kupitia kwetu.
1Timotheo 4:12 “Mtu awaye yote asidharau ujana wako,bali uwe
kielelezo kwao waaminio,katika usemi na mwenendo na katika upendo na imani na usafi”
Habari zote tunazotoa katika vyombo
vya mawasiliano,zinapaswa kuwa zenye ukweli na zinazo mjenga msomaji,msikilizaji
au mtazamaji na zenye kuhimiza imani ya dhati,utakatifu na ukweli.
CHANGAMOTO
Ewe
Mwanafunzi,mwanachuo uliyepo katika mazingira ya chuoni unatumiaje vyombo hivyo
vya mawasiliano?Unawasiliana nini na wenzako kupitia vyombo hivyo? Kama; simuzamkononi,e_mail,face_book,twitter,lap_top
na vyombo vingine? Je unawakumbusha
wenzako mambo ya kiroho kupitia vyombo
hivyo,kujulisha upendo wa Yesu na kumweka rafiki yako karibu na msalaba wa
Yesu?
Au unatumia vyombo hivyo kwaajili ya umbea,masengenyo,udaku,kutumiana
meseji za mapenzi(uasherati&uzinzi) na mengine yafananayo na hayo?
katika makundi tunayo soma(group discussions)
ni ujumbe upi tunawapatia wenzetu? Kumbuka
tupo katika kipindi cha mwisho cha kuelekea kufunga historia ya ulimwengu.
Jihoji!!!...... Tafakari
Tunapaswa kujua uhuru wa kuwasiliana
ukizingatia maadili ya mawasiliano,uwazi na uaminifu.
Hivyo waajiri,waajiriwa,wanachuo,wanafunzi
na watu wote tunapaswa tujue uwazi,uwaminifu na kuwa na mahusiano ya karibu
yenye kujenga.
FAIDA ZA MAWASILIANO
1.Mawasiliano
mazuri yanaweza kukufikisha katika mafanikio makubwa kwa kuwa na mahusiano
mazuri kijamii na watu wengine bila kujali matabaka walionayo,utapata elimu kwa
kubadilishana mawazo na kukua kitaaluma unapo jishirikisha na kujihusisha
katika mashirika mbalimbali.
Mungu
ametufunulia kutambua nyakati,ishara na matukio mbalimbali. Mfano: dalili za kurudi kwa YESU mara ya pili Mathayo
24:3-14.ishara ya upinde wa mvua baada ya gharika n.k.
Mwanzo 11:11 “Na agano langu nalithibitisha nanyi,wala kila
chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika,wala hakutakuwa tena
gharika,baada ya hayo kuiharibu nchi”
2.Mawasiliano yanatusaidia kudai
ahadi zetu,dhidi ya wale tunao wasiliana nao.Mfano: kupitia maombi yetu na MUUMBAJI wetu tunaweza kudai ahadi
zetu kwake.
Wafilipi 4:6 “Msijisumbue kwa neno lolote bali katika kila neno
kwa kusali na kuomba haja zenu na zijulikane
1.Kupitia vyombo vya mawasiliano
tunaweza kuvunja kwa MUNGU”
HASARA ZA KUTUMIA VIBAYA MAWASILIANO.
sheria
ya MUNGU (amri kumi za Mungu)waziwazi.
Mfano:kusema uongo,umbea,kusengenya,kutamani,ufisadi,rushwa,kutumiana
meseji za mapenzi(uzinzi&uasherati),kuangalia ponographical pictures na
mengineyo.
Hali
kama hii inapaswa kukemewa mara moja na kuepukwa kabisa.
2.Upotevu
wa mali nyingi kupitia vyombo hivyo bila kuona mafanikio yake.
3.Kuharibu
ndoto au njozi za maisha yako,kushindwa kufika pale unapo takiwa kufika. Mfano: mimba zisizo tarajiwa,ndoa ambazo
hazijapangwa au zisizotarajiwa.
4.Upotevu
wa muda kwenye vyombo hivyo vya mawasiliano kama vitatumiwa vibaya hasa katika
e-mail,facebook,twitter na vingine.
5. Mavazi
na usemi wetu vyaweza kuondoa uwepo wa roho mtakatifu katika maisha
yetu.Tunabaki bila roho wa Mungu,HASARA
ILIYOJE!!.
Wakolosai 1:10-11
WITO
Tuendelee kudumu kuwa na mawasiliano mazuri na
MUUMBAJI wetu,watu wanao tuzunguka katika makazi yetu(nyumbani)kazini na
masomoni pia.TUTABARIKIWA.
Somo la 2.
KUTEMBEA KATIKA BARABARA YA UTAKATIFU USIO NA
HILA.
Utakatifu maana yake ni kutokuwa na dhambi yoyote.ni kuwa
mweupe na safi kabisa kwa kila jambo. Na Biblia inatueleza kwamba Mungu peke
yake ndiye mtakatifu.
ZAB 99:9è”Mtukuzeni Mungu wetu; sujuduni mkiukabili
mlima wake mtakatifu; Bwana Mungu wetu ndiye mtakatifu.
Tunapaswa kumtukuza Mungu wetu na kumtolea ibada kwa kua
yeye anastahili kuabudiwa nasi tu kazi ya mikono yake.
UFUNUO: 4:8 è”Na hawa wenye uhai wanne kila mmoja alikuwa
na mabawa sita na Pande zote na ndani
wamejaa macho na wala hawapumziki usiku na Mchana, wakisema Mtakatifu Mtakatifu
Bwana Mungu mwenyezi Aliyekuwako aliyeko na atakayekuja.
Hakika Mungu
anastahili kuabudiwa.Kama viumbe walioko mbele zake hawachoki wala
hawasinzii, ibada kwa Mungu ni masaa ishirini na manne na wala hawatoi udhuru,
na wala hawakuanguka katika dhambi, lakini wanaishi kwa kumtukuza Muumba wao. Je wewe na mimi tunafanya hivyo? Viumbe
wa mbinguni wanajua faida za kumtolea Mungu Ibada kama stahili yake!
ISAYA 57:15 è “Maana
yeye aliye juu aliyetukuka akaaye milele
jina lake ni mtakatifu asema hivi.”Nakaa mahali
palipoinuka palipo patakatifu, tena pamoja na yeye aliye na roho za
wanyenyekevu na kuifufua mioyo ya watu”. Toba katika maisha
yetu ni suluhisho la sisi kukubalika mbele za Muumbaji wetu 1Petro1:15-16 “Bali kama yeye aliyewaitwa alivyo mtakatifu nanyi iweni watakatifu
katika mwenendo wenu wote kwa maana imeandikwa, mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi
ni mtakatifu”.
Vijana wa
Kiadentista wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa mahali popote wawapo. Wajione kuwa
wao ni mawakili wa siri za Mungu katika tabia na mienendo yao ili kanisa la
Mungu lisitukanwe; Wajione kuwa wao ni wabeba nuru kati ya giza la utandawazi unaoitumbukiza dunia katika
tabia isiyofaa wala kumtukuza Mungu wa
mbinguni. Wajione kuwa wao ni hazina ya kanisa la Mungu popote walipo.Mungu
huchukia dhambi hata wenye dhambi hawawezi kushirikiana naye ZAB 5:4,”Maana
huwi Mungu apendezwaye na ubaya; mtu mwovu hatakaa kwako”.
ZAB.15:1-3 è “Bwana
ni nani atakayekaa katika hema yako? Ni nani atakayefanya maskani yetu katika
kilima chako kitakatifu? Ni mtu aendaye kwa ukamilifu na kwa kutenda haki. Asemaye
kweli kwa moyo wake, asiyesingizia kwa
ulimi wake, wala hakumtenda mwenziwe mabaya, wala hakumseng’enya jiani yake”.Mungu
wa mbinguni asiye na hila
hutamani watu wawe mfano wa kuigwa ambao matazamio na makusudi yao ni kuishi
pamoja na Mungu katika ufalme wake;
“kuwa
miongoni mwa watu hao”. Mungu alikataa kuwasaidia Waisraeli walipokuwa pamoja na
wenye dhambi, yaani Akani mwana wa Karmi Yosh 7:1,10-12.
Watu wasiofaa wenye dhambi kama Akani wanaweza kuwa mzigo
kwa ndugu,dada na wanaosafiri safari ya matumaini. Lakini mmoja wetu aweza kuwa
kikwazo cha Mungu kutokuwa upande wetu. Je,wewe ni Akani utabishaye kundi
hata Mungu hataki kusikia maombi yetu?
Mungu hutoa mwito kwetu leo 2 kor 6: 17- 18 “Kwa hiyo tokeni kati yao
mkatengwe nao asema BWANA, msiguse kitu
kilicho kichafu,nami nitawakaribisha, nitakuwa Baba kwenu nanyi mtakuwa kwangu
wanangu wa kiume na wa kike asema Bwana Mwenyezi.”
Tunatakiwa tumwone Mungu katika maisha yetu ya kila siku.Naamini hatutabaki kama tulivyo. Musa aliomba
aonyeshwe utakatifu wa Mungu Kut 33:18-23.
Mungu alikuwa tayari kumwonyesha utukufu wake kwa sharti
la kumficha kwenye mwamba ili asidhurike.
Tutakapotamani kukaa pamoja na Mungu, Mungu yuko tayari kutuficha katika
mwamba wake, yaani Yesu kristo atatufunika kwa haki yake ili tustahili
kusimama pale.
Isaya alipomwona
Mungu akaona mapungufu yake akatamani kubadilishwa ili akubalike
mbele zake. Mungu alikuwa tayari kumtuma malaika kwa ajili ya huduma kumtakasa.
Vivyo hivyo nasi Mungu yuko tayari kwa ajili ya kubadilisha mielekeo yetu miovu
kwa njia ya utakaso Isaya
6:1-5.
Mungu ni mtakatifu na utakatifu usio kuwa na hila wala
hitilafu yoyote.Imetupasa Sisi kukiri
kwamba ndivyo alivyo, na tena hatuwezi kumkaribia tusipotakaswa Maovu yetu kwa
njia ya kumkubali Yesu Kristo pale msalabani kama mbadala kwa ajili ya dhambi zetu.
kwa nini usitoe maisha yako kwake ili utembee katika
barabara ya utakatifu usio na hila?
Kusudia moyoni mwako tangu sasa.
SOMO la 3.
MUNGU ANAYEJALI
-
Wana wa
manabii ambao walikuwa katika shule za manabii walikuwa wakikaa pamoja.Na Mungu
alikuwa akiwafunulia mambo ambayo alipenda wayafahamu. 2Wafalme 2:3-4.
-
Hapa
tunawaona Eliya pamoja na Elisha. ”Elisha akasema kama Bwana aishivyo na roho yako iishivyo sitakuacha:Basi
wakashuka mpaka Betheli:Basi wana wa manabii walio kuweko Betheli wakamwambia
Elisha: Je unajua kuwa BWANA atamwondoa bwana wako leo asiwe mkubwa wako?”
Wana wa manabii ambao
walikuwako Yeriko walifahamu jambo hili la kuondolewa ELIYA.-soma 2Wafalme 2:5.
HEBU TUANGALIE KISA KUTOKA KWA WANA WA MANABII.
2Wafalme 6:1-7.
Fungu la 2Walme 6:3- Mmoja
wa wana wa manabii akasema “Uwe radhi,basi nakusihi uende pamoja na watumishi
wako.”Akajibu nitakwenda.
· Kazi ya kukata miti ya
ujenzi ilianza lakini akatokea mmoja wapo wa wale watoto wa manabii shoka yake(boriti) ilizama katika
maji. 2Wafalme 6:5.
Mambo yaliyo mpata baada ya kupoteza ile shoka:-
®
Hofu na
mashaka vilitawala moyo wake.
®
Hakujua
namna ya kuweza kuitoa katika maji.
®
Shoka
ilikuwa ni ya kuazima. Angesema nini juu ya mwenye shoka? 2Wafalme 6:5b.
®
Alisahau
kuwa alikuwa na mtumishi wa Mungu.
“Mungu anaye jali aliyaona yote yaliyo msumbua huyu kijana”.Ndipo roho wa Bwana
akamtumia nabii Elisha, “kilianguka wapi…?”,Akamwonyesha mahali.Akakata kijiti akakitupa palepale
chuma kikaelea. 2Wafalme 6:6
Ni
fundisho gani tunalipata katika kisa hiki?
(a). Mungu alijishugulisha na
mkasa wa kukitoa chuma cha boriti ya shoka kupitia kwa mtumishi wake Elisha
(b). Mungu wetu yuko tayari
kusikia hitaji la kila mmoja wetu,hajali kuwa wewe ni mtu wa namna gani.
(c). Wana wa manabii walikuwa
tayari kusikia na kutekeleza kile alichosema Nabii 2Wafalme 9:1-6
(d). Wana wa manabii wakiwa
katika shule na vyuo vya manabii walijifunza neno la Mungu, hata kutabiri.
{GILGALI, BETHELI NA YERIKO: 2Wafalme 2:3,5,15, 4:38}
MASWALI YAKUTAFAKARI
(i)
Je sisi
tunaojiita Wakristo, tuko tayari kuongozwa na Roho Mtakatifu?
(ii)
Misingi
ambayo Mungu aliiweka kwa manabii wake imetuonyesha jinsi wana wa manabii
walivyojihusisha na neno lake, pia kumtegemea. Je sisi wana vyuo, misingi ya vitabu vya neno la
Mungu tunaisimamia vyema?
(iii)
Je imani yako leo imejengwa kwa nani?
(iv)
Neno la
Mungu linasema inunue kweli wala usiiuze Mithali 23:23
Je umeinua kweli? Yaani maandiko
matakatifu unayasoma na kuyafanya kuwa taa yako ya Maisha?. Zaburi 119:105
WITO.
Iwapo mungu akijali chuma kilichopotelea majini na kuweza
kutenda mujiza kikaelea,mungu huyo pia anajali maisha yako,anajali elimu
yakounapoyaamini maandiko matakatifu.
2 Timotheo 3:16-17
“ASANTE MUNGU WETU ANAYEJALI AKUBARIKI”.
SOMO la 4.
MWADVENTISTA NA MTINDO WA MAISHA KATIKA MAZINGIRA YA CHUO.
Fungu kuu Warumi 12:1-2
UTANGULIZI.
Lengo
la mada hii ni kuibua mjadala
mpana katika kile kinachoitwa mtindo wa maisha na athari zake kwa maisha ya
vijana waadventista wa Sabato chuoni, hivyo kwa kifupi,mada chache tu katika
eneo hili zimeguswa kama kichokoo kutupeleka katika mjadala wa kina dhidi ya
mada hii.
Mtindo wa maisha (life style) ni jumla ya mambo yote yanayohusiana na namna
ya ulaji, unywaji, matumizi ya pesa, mavazi na uvaaji, matembezi (outings),
muziki, matumizi ya vyombo vya mawasiliano kama;simu za mkononi, ipod, runinga,
tovuti, Email n.k katika maisha ya kila siku ya
familia au jamii.
Nukuu: According
to www.businessdictionary.com/definition/lifestyle “Lifestyle
is expressed in both work and leisure behavior patterns and (on an
individual basis) in activities, attitudes, interests, opinions, values, and allocation of income. It also reflects people's self image or self concept; the way they see themselves and believe they are seen by
the others. Lifestyle is a composite of motivations, needs, and wants and is influenced
by factors such as culture, family, reference groups, and social class”.
Kuna changamoto kubwa sana katika ulimwengu wa leo,hususan
tunapozungumzia dhana ya mtindo wa maisha. Suala hili halikomei katika
kuajadili kumomonyoka kwa maadili peke yake, bali pia hugusa kwa kiwango
kikubwa wajibu wa kiroho kwa kila mmoja wetu, kwani athari zake zinaonekana
wazi katika maisha yetu.
Inaonekana
dhahiri kuwa, mitindo ya maisha inazidi kuleta athari kubwa za kimwili, kiakili na kiroho kwa vijana wetu hususan walio katika taasasi
za elimu ya juu, hasa vyuo vikuu na vyuo vya kati. Hali hii inachangiwa kwa
kiwango kikubwa na upanukaji wa mawasiliano yaliyopelekewa na kutapakaa kwa
utandawazi ambao kwa namna moja au nyingine umeleta athari kubwa za kiuchumi, kisiasa, na kijamii hivyo
kuathiri mtindo wa maisha na kusababisha vijana wetu kujaribu kupambana na
athari zake kwa kuiga mitindo ya maisha
ya magharibi amabayo kwa namna moja inaonelewa kuwa ndio mitindo bora ya maisha
kwa makundi rika yaliyo mengi duniani.
MTINDO WA MAISHA YA ULAJI NA UNYWAJI.
1Wakorintho 10:31,Mithali 16:3, Mithali 20:1,
Danieli,Shadrack,
Meshack na Abedinego (Dan
2-3), Musa na Yusufu wanabaki kuwa kielelezo bora cha wasomi wa kale
waliofanikiwa sana katika kumtetea Mungu wakiwa ndani ya taasisi mbalimbali za
kielimu na utumishi katika nchi za ugenini.Haikupata kutokea wakaathiriwa na
mitindo ya maisha kiasi kwamba wakamwacha Mungu na kugeukia anasa kama vijana
wetu leo.
Ni dhahiri
kuwa, baadhi ya vijana wetu katika vyuo vya elimu ya juu na kati, wamedhihirika
kushiriki sana ulaji wa vyakula najisi pamoja na unywaji wa vileo mbalimabli
kama vile bia,(beer) na vingine vinavyo sisimua miili yao,(Counsels on health pg450) Mambo haya yamechangia kwa kiasi kikubwa
vijana wa aina hiyokukwepa sana kujiunga na vyama vya vyuo kama THISDASO mara
wanapoingia chuoni. Matumizi haya ya anasa na vyakula najisi pia hudhihirika
katika shughuli za mahafali pale vijana wetu wanapohitimu masomo yao, mambo haya hufanyika kwa siri katika kumbi za starehe au
katika mahoteli na migahawa ya kisasa,(selected messages vol.3 pg 287,
Patriarchs’ and Prophets pg562). Hali hii huchukuliwa na wanafunzi kama kiwango cha juu cha ustaarabu na usasa. Kuzoelea
anasa huku kumehafifisha sana makuzi ya kiroho kwa vijana wetu walio wengi
ambao kwa taaluma zao,wanatarajiwa hapo baadaye kushika nyadhifa mbalimbali za
kanisa ili kulivusha katika changamoto kubwa hizi za maisha ya kiroho,kimwili
na kiakili. Je wewe ni mmoja wao na
ni hatua gani unachukua kukabilina na changamoto hii?
MTINDO WA MAISHA, MAVAZI NA MATUMIZI
YA PESA.
1Timotheo 6:10,Mathayo 6:22-23
Matumizi
ya anasa yamesababisha vijana walio wengi kutamani pesa kwa kiwango kikubwa,
hali hii imekumba vijana wetu walio wengi. Pesa imekuwa chanzo cha vishawishi
vingi hususani ngono, ulevi, ulafi, mavazi ya garama na anasa za matembezi
yaitwayo(outings) pamoja na (picnics) ambayo yamechochea mazoea ya U-Boy friend
na U-girl friend unaoishia katika mimba zisizotarajiwa au kuaibishana na
kudhalilishana kwa wapenzi hawa ambao hawakutarajia ndoa hizo za mapema.
Pesa
imekuza uadui baiana ya mtu na mtu na imechochea,chuki,husuda,kijicho,umbea,unafiki,wivu,mauji,magonjwa
kama UKIMWI na kukosa subira. Na Kwa jinsi hiyo wengi wamenaswa katika mtego wa
yule mwovu kiasi cha kushindwa kusimama imara juu ya mwamba ambaye ni
kristo.Imani wameiacha na kujikuta wakiwa mawakala wa shetani katika mazingira
ya vyuo vyao. Nijukumu la vijana wetu kutambua kuwa kutamani pesa sana kuna
leta athari kubwa kwa maisha ya kijana mwadventista. Yatubidi kuwa na kiasi na
kutambua uwezo wetu. Si vyema kutamani matumizi
ya pesa yanayozidi kiwango cha kipato chetu kwani madhara yake ni
makubwa mno katika maisha yetu. Chukua hatua jifunze madhara ya pesa kupitia
kisa cha YUDA ISKARIOTE.
Lakini pia mitindo ya mavazi ya kimagharibi kama vile
uvaaji wa suruali kwa mlegezo au (KK) kama inavyojulikana,sketi za kubana,
vi-body, vi-top, stretcher-trouser, mitindo ya kusuka nywele na matumizi ya
Mecuric-creams au Mikorogo kwa ajili ya kuchubua ngozi vinazidi kushika kasi
kwa vijana leo kanisani.Hali hii haiwezi kuachwa tu bila ya kukemewa
na kanisa, hasa pale kanisa linapo jiaandaa kumlaki Bwana Yesu hivi punde.
Tamaa hizi mbaya lazima zionywe kwa neno la Mungu (Evangelism pg 272, Child guidance 429,430). Aina hii ya mavazi na
uvaaji ni lazima ipigwe marufuku katika makusanyiko matakatifu. Vijana wasaidiwe
kwa hekima kuona ubaya wa mivuto hii isiyokubaliana na imani yetu.
MTINDO WA MAISHA NA MATUMIZI YA
MUZIKI NA VYOMBO VYA MAWASILIANO.
Warumi 8:4-8
Katika
Nyanja ambazo shetani amejipatia wateja wengi leo ni hii ya muziki na vyombo
vya mawasiliano.Leo muziki umekuwa mojawapo ya mahitaji ya msingi ya binadamu.Katika
kizazi hiki,muziki, hasa ule wa kimagharibi umekuwa ukitukuzwa na kuingizwa
katika baadhi ya ibaada za madhehebu ya kikikristo, lakini pia si ajabu
tamaduni hizi za kishenzi zimaenza kupenyezwa hata ndani ya kanisa la
Mungu,inatubidi kuchukua tahadhari kubwa tunapo chagua nini cha kusikiliza.(Education pg 167-168, Testmonies vol 4,pg
652-653)
Isitoshe
leo kunavijana wetu wa kiadventista wanahudhuria katika kumbi kubwa za muziki
na kukesha huko wakimtumikia mwovu,mazoea haya yameathiri tabia zao njema na
kuua imani na uhusiano wao na Kristo Yesu.
Hata
hivyo matumizi ya simu za mikononi, laptop na tovuti ni mojawapo ya mitindo ya
maisha inayoleta madhara makubwa kwa vijana wetu. Tovuti badala ya kuwa vyanzo
vya taarifa za masomo, vijana wetu walio wengi wamekuwa wakivitumia kama njia
ya kujifunza mambo machafu ya ngono ambayo yanaathiri sana mwelekeo wao maisha
ya baadaye hususani katika maisha yao ya ndoa(1 wakorintho 6:8).
Vivyo
hivyo simu za mikononi nazo pia zinatumika kwa makusudi kama hayo ikiwa ni
pamoja na kupashana ujumbe wa mapenzi au kuchochea ashiki za kingono. Mambo
haya yasipoepukwa hayatamwacha salama kijana mwadventista.Mkazo uwekwe
kwa kiwango kikubwa katika kusimamia na kuhamasisha vijana wetu kuishi maisha
matakatifu yanayompendeza Mungu.
WITO.
Wakati
umefika kwa vijana wetu kuamka katika usingizi wa kiroho na kupambana na hali
hii mbaya inayodhoofisha ukuaji wa kiroho kwa vijana wetu. Tukiwa wasomi katika
taaluma mbalimbali ni vyema basi tutumie elimu zetu kwa uangalifu huku
tukimwinua Yesu juu kupitia maisha yetu ya kimwili,kiakili na kiroho.Nikujidanganya
bure kudhani kuwa unajua unachokifanya,Bwana anonaye sirini ataleta kila jambo
hukumuni liwe jema au liwe baya.Wapo wengi wenye hekima na wasomi waliobobea
katika Biblia ambao walidumu kumcha Mungu pamoja na hadhi zao,na Bwana
aliwainua juu sana na kuwakweza kama alivyotenda kwa Musa pale Misri.
Kama
kijana Mwadventista unapaswa kuwa kielelezo ndani ya kanisa,ndani ya maeneo ya
chuo chako, katika kundi lako la kujisomea, na jamii kwa ujumla, jihadhari
kumtweza roho wa Mungu pale anaponena nawe leo.
Chagua kufanya matengenezo ya kweli.
SOMO LA
5.
KIOO CHA
AJABU.
(SHERIA YA MUNGU ISIYOBADILIKA)
FUNGU
KUU:
“Sheria ya BWANA ni kamilifu, huiburudisha nafsi, Ushuhuda wa BWANA ni amini,
humtia mjinga hekima”. Zab
19:7
Ni jambo la pekee na lenye
faida kubwa kuwa,mtu aishikaye sheria ya Mungu anakuwa ni mwenye amani, furaha
na mwenye uhakika wa kuuingia mji mtakatifu – Mbinguni.
‘Twaweza kujiuliza nini maana ya sheria………….?’
Sheria ni utaratibu, agizo
au mwongozo wenye mamlaka uliotolewa na mwenye mamlaka kwa ajili ya kutoa
maelezo sahihi kwa jamii katika kuelekeza, kusimamia, kukosoa na kuadibisha.
Sheria ya Mungu inafananishwa
na kioo kwa maana hii kuwa,ina uwezo wa kuonyesha bayana / kwa usahihi uovu au
makosa ya mwanadamu. Kwa sababu sheria yake ni kamilifu, inaonesha kwa usahihi
usiokuwa na shaka yoyote kuwa dhambi ni hii na utakatifu ni huu. Yakobo 1:23, Warumi 2:13
Ila sheria yenyewe haina uwezo wa kuondoa dhambi/makosa –
kama kioo kilivyo.
Maneno haya: sheria, Amri na torati katika maandiko matakatifu (Biblia) wakati mwingine hutumika
katika ulinganifu au kwa maana sawasawa.
Mfano. Soma aya hizi; Zab. 19:7, 1Yoh 5:3, Rum 7:7,
Zab1:2, Yoh 14:15.
KAZI ZA SHERIA
Ndugu zangu wapendwa
ninapenda tufahamu kuwa sheria ya Mungu ina kazi hizi zifuatazo (japo waweza
kufahamu ngingi zaidi);
1. Kuifanya dhambi
ionekane/kuitambulisha dhambi. Rum 7:7-13
2. Kutuongoza kwa Kristo
(Sheria ni kiongozi) Gal. 3:24
SHERIA NA NEEMA
Ni kweli kuwa tunaokolewa
kwa neema, ambayo hutuongoza kuikataa dhambi. Na hatuwezi kuitambua dhambi
pasipokuwa na sheria.Naam, sheria huionesha/funua dhambi
na Neema ya Kristo huiondoa. Tito 2:11-12.
MAKUNDI YA SHERIA
Katika Biblia, sheria
yaweza kufundishwa katika namna nyingi au makundi tofautitofauti.
Hebu tuyatazame makundi
makuu haya mawili.
(1). Sheria zilizoandikwa na
Mungu, muumba wa mbingu na nchi.
(sheria/amri
10 za Mungu)
(2). Sheria zilizoandikwa na
Musa, Nabii wa Mungu
(sheria za maagizo).
(1).SHERIA ZA MUNGU (Amri 10)
Hii inaitwa sheria ya Mungu
isiyobadilika kwa sababu, Mungu habadiliki badiliki, yaani hana kigeugeu, na maneno
yake ni amini. Hes. 23:19, Yak 1:17, Tito 1:2 na 1Sam 15:29
Sifa za sheria za Mungu.
(i)
Ziliandikwa
na Mungu mwenyewe kwa chanda chake.Kut.24:12, 31:18, Kumb. 9:10
(ii)
Ziliandikwa
katika mbao mbili za mawe Kut. 31:18
(iii)
Zilitunzwa
ndani ya sanduku la agano. Kumb. 10:1-2
(iv)
Nakala
ya sheria hiza iko mbinguni. Uf. 11:19
(v)
Zitatumika
katika hukumu siku ya mwisho.
Ndizo
zitakazokuwa kipimo katika hukumu ya Mungu ijayo
·
Yak
2:10-12 - Tutahukumiwa kwa sheria ya uhuru
·
Math.
19:16-19 – Ukitaka kuingia mbinguni, zishike amri
·
Rum 2:13
– Zishike amri.
“Watakaoingia mbinguni ni wale tu
wayafanyao mapenzi ya Mungu,na mapenzi ya Mungu ni kuzishika amri zake. Mith.
7:20, Yoh 14: 15”.
(2).SHERIA ZA MAAGIZO
Kwa uongozi wa roho mtakatifu, sheria
hizi ziliandikwa na Musa,na zina sifa hizi:
(i)
Mwandishi
wake ni Musa (Nabii wa Mungu)
Kumb
31:9
(ii)
Ziliandikwa
katika chuo/magombo/magome ya miti yaliyotengenezwa kwa ustadi. Kumb. 31: 24
(iii)
Zilihifadhiwa
kando ya sanduku la agano lililokuwa na amri kumi (10) za Mungu. Kumb. 31: 26.
Sheria za maagizo zilihusu mambo haya:
(a). Tohara (Mwanzo 17:9-11)
Sheria hii ilifikia ukomo
wake, kwani ilikuwa ni mfano kivuli. 1Kor. 7:19, Rum 2: 28-29
(b). Kafara ya wanyama (Walawi
16:15)
Sheria hii ilifika ukomo
pale msalabani kwa sababu ya kafara ya Yesu Kristo, Luka 23:44, 45, 1Yoh. 1:7,
Rum 5:9, 1Pet 1:19
(c). Ndoa (Walawi 18:20-22)
Sheria hii inaendelea.
Ebr. 13:4, Kut. 20:14
(d). Mavazi (Kumb. 22:5)
Sheria hii inaendelea.
1Tim 2:9
(e). Afya (Walawi 11,
Kumb.23:12-14)
Mungu anahitaji tule
kilicho chakula (walawi 11) na kuyaweka mazingira safi (kumb. 23:12-14)
Sheria hii inaendelea.
(1Kor.3:16-17, 6:19-20
(f). Zaka na sadaka (Walawi 27:
30-34)
Twapaswa pia kulitekeleza
agizo/ amri hii. Malaki 3:10
(g). Sikukuu (Walawi 25)
Ziko sikukuu zilizofikia
ukomo na zingine zinaendelea. Mf. Isaya 66:22-23, kut. 31:12,17, Ezek 20:12,
kumb. 16:13-19, Zek. 14:16
SHUGHULISHA UBONGO:
Rafiki wasafiri wenzangu, napenda
tufahamu jambo hili kuwa, kuikataa sheria ya Mungu ni kuukataa mpango mzima wa
wokovu
Hebu tazama kielelezo hiki:
(1). Sheria
(2). Dhambi
(3). Mhubiri
(4). Injili
(5). Mwokozi
(6). Kanisa
(7). Wokovu
“Pasipo SHERIA
hakuna DHAMBI (Rum 7:7). Na kama hakuna dhambi,
hakuna hitaji la MHUBIRI/WAHUBIRI maana wao huihubiri INJILI inayomhusu
MWOKOZI (Yesu Kristo) anayeikataa dhambi.
Watu wanapoisikia injili na kumpokea
mwokozi huja KANISANI wakifanywa tayari na kujiandaa kuupata
WOKOVU”.
HITIMISHO.
Watu wengi leo wanafanya jitihada za
kila namna kutii sheria za wakubwa wao wa kazi, waajiri wao ama wasimamizi wao
wenye mamlaka. Sheria hizi zinazingatiwa sana na kupewa heshima na nafasi
kubwa.
Mfano. Wanafunzi shuleni au vyuoni, huzingatia sheria
za vyuo ili wasifukuzwe vyuoni. Huzingatia sheria za mitihani kama; kuwa na
kitambulisho cha mtihani, kuwa na vifaa vyote vya mitihani na hata vya ziada,kutokuwa
na/kuto kukutwa na chanzo chochote cha majibu mf.karatasi(Nondo) n.k.
Kwa nini
tusitie bidii kuzishika amri za Mungu wetu, tena kwa kutetemeka? Je Mungu si zaidi sana ya wanadamu hao tunaowaogopa kwa kuzizingatia
sheria zao……….?“Tafakari ………………………!!
WITO:
Hebu ikubali sheria ya Mungu:
Tusipozingatia amri za Mungu, Kweli
haimo ndani yetu hata kidogo 1Yoh 2,4 pia Sala zetu ni chukizo. Mith 28:9.
SOMO LA 6.
KWANINI UAMSHO WA KISASA HAUJAFAULU..?
Neno Uamsho ni neno zuri linaloleta maana halisi ya
mpango wa kumwokoa mtu aliyekwama mahali Fulani kiroho, mtu ambaye kamwe hawezi
kujikwamua bila kupata msaada toka nje ya uwezo wake.
Mada hii kiasili
imekuwepo tangu mwanadamu alipoanguka na kama ingetokea kwa bahati mbaya kizazi
fulani kipite bila wacha Mungu kufanya Uamsho kwa msaada wa Mungu wao, basi
kizazi hicho kingelipita bila Mungu kujipatia watu wake, na Mungu angaliweza
kudharauliwa milele.
Maneno haya
yanaonyesha kwamba mtu wa kwanza kushikilia jukumu hili na kufanyia kizazi
chake Uamsho mkubwa-alikuwa ni Adamu.
-
Kwa muda wa miaka karibu
Elfu moja Adamu aliishi miongoni mwa watu akiwa shahidi kwa matokeo ya dhambi, alikuwa ameagizwa
kuelekeza vizazi vyake vijavyo katika njia ya Bwana na kwa uangalifu alitunza
kile ambacho Mungu alikuwa amedhihirisha
kwake,na alikirudia kwa vizazi vilivyofuata kwa watoto wake, wajukuu
zake hadi kizazi cha tisa alieleza hali ya furaha na takatifu ya mwanadamu
katika paradise.Alirudia historia ya anguko lake akiwaelezea njia za huruma kwa
ajili ya wokovu wao, na bado ni wachache tu walijali maneno yake. Mara nyingi
alikutana na Malaumu kwa dhambi ambayo ilileta shida kama hiyo kwa vizazi vyake
vijavyo. (Patriaches&Prophets. uku
82 aya II).
Nabii anadhibitisha jinsi adamu alivyokuwa mwaminifu
katika kufanya uamsho lakini pia anataja majukumu aliyokutana nayo na hii ndiyo shida inayokikuba kizazi cha
leo. Watu wa kizazi cha Adamu pamoja na kukataa Ukweli wa
uwazi uliokuwepo wazi mbele yao na Adamu mwenyewe, lakini bado walikuwa
hawajafikia mambo makubw a ya ubunifu tunayoshuhudia leo. Ukiachilia mbali
Elimu tuliyonayo, leo makanisani huwezi kuamini kwamba ni mahali panapotajwa
jina takatifu la BWANA yeye ambaye tunajifunza kwake kwamba kila kitu kilitoka
mikononi mwake wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilchofanyika Yohana
1 : 1 – 4.
Yeye ambaye viumbe vitakatifu ambavyo havikuanguka
vinamwabudu kwa hicho usiku na mchana bila kukoma na makerubi wakifunika nyuso
zao kwa mabawa yao,Ufunuo 4 :8-11.
Huyo sisi tumemfanyia Uamsho wa bandia tukitumia
jina hilo hilo takatifu,tunacheza na
kubakia uchi tunashangilia kwa makofi na vigelegele, tumeshuhudia hata vuvuzela
kwenye baadhi ya nyumba za ibada,…….. ajabu ilioje!!
Tunachohitaji kutafuta hapa ni, kwa nini Uamsho wa kisasa unashindwa kufaulu?
Kama hapa
tungalikuwa na muda wa kotosha tungaliweza kuzama na kuangalia kizazi hadi
kizazi tuone ni wapi walipofanya vibaya nani wapi walipofanya vizuri lakini
wewe kama mshiriki na mwanafunzi binafsi
unao muda wa kutosha kufanya hayo yote, na zaidi hebu usilale, fanya kitu
katika zamu yako. Habakuki 2 :1 -2
Kanisa la Mungu
duniani limepewa jukumu zito la kuhakikisha kila anayeitwa mwanadamu ameambiwa
habari juu ya wokovu wake na kama anazo
habari hizo tayari anaamshwa kundelea na safari.
Bila kufanya hivyo wengi watachanganyikiwa katika kizazi
hiki lenye ukaidi ambapo kuna dhana mbalimbali ikiwemo dhana potofu inayo ila
Dunia sasa hivi- dhana ya upako ambayo Inabeba mambo mawili makubwa
ndani yake;
Moja uponyaji na ya Pili utajizisho. Mambo ambayo kiasili
hayakataliwi na maandiko lakini adui ameazimia kutumia
mambo haya kama ndoano na Hakika amefaulu na kuwanasa walio wengi.
Ukweli ni kwamba wote katika vipindi vyote waliyofanya
Uamsho wa kufaulu walijitenga mbali na mambo haya yote wakatambua dunia ya wakati wao, wakamweka Mungu
kuwa wa kwanza katika mambo yao yote.
·
Mwanngalie Yusufu kule misri ,
·
Mwone Danieli na wenzake wakiwa kule Babeli ,
·
Mwone Yeremia akisimama peke yake katika
wakati mgumu
·
Vipi Eliya mitishbi wakati wa ibada ya Miungu!
Tuwaone wanafunzi walioishi katika kipindi kigumu cha utawala katili wa Rumi, walihitimisha historia
kwa ushindi mkuu wakimwinua Kristo mfufuka hata kama kama walikatazwa kufanya hivyo.
Kazi imebakia kwetu lakini Hatuwezi kufanya hivyo kama
Hatutakubali kuondoa tofauti zetu na kuungana na kuwa wa sauti moja.Mkulima
akifanya sehemu yake, mfanya biashara naye katika biashara yake, Mwanachuo naye
kama Mwanachuo kwa sehemu yake.
Kumbuka mwanachuo- kama Musa kwenye Ikulu ya Farao,
Mungu amekaa kimya anasubiri kuona unamwakilishaje hapo ulipo, na hata wakati
mwingine unalazimika ushuke kwenda kuwaangalia watu wako wanaoteseka, hiyo ni
sehemu ya uamsho.
Bwana atakuwa
msada wako-Uamsho wako utafaulu nawe utabarikiwa.
“Shuka sasa shuka leo Uwaone”.
Amina.
“MARANATHA…..!!!”
No comments:
Post a Comment