TANZANIA HIGHER
LEARNING INSTITUTION SEVENTH-DAY ADVENTIST STUDENT ORGANISATION (THISDASO),
DODOMA ZONE.
IDARA
YA MAMBO YA KIROHO – KANDA YA DODOMA.
Tarehe 02 – 10/06/2012.
Karibuni wageni Kwa wenyeji
tuyachunguze maandiko.
SOMO LA KWANZA: MAHUSIANO SAHIHI.
SEHEMU YA KWANZA. Juma Pili - 03/06/2012.
UTANGULIZI
Maana ya uhusiano, Uhusiano ni neno pana sana kutegemea mahali
linapotumika, kamusi ya Kiswahili sanifu inaeleza uhusiano kuwa ni hali ya kuwa
na mfungamano.Kuna uhusiano mzuri au sahihi na uhusiano mbaya. Uhusiano ni tabia ya MUNGU, YESU anasema “Mimi na BABA tu umoja” Yoh 10:30, “kwa maana wako watatu washuhudiao mbinguni; Baba, Neno na Roho Mtakatifu
na hawa wote ni umoja” 1Yoh 5:8, umoja kati ya nafsi hai za
uungu ni udhihirisho wa uhusiano mtakatifu katika tabia na utendaji kati ya
MUNGU Baba, Mwana na Roho mtakatifu.
Kwa kuwa mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa MUNGU
aliumbiwa tabia hii ya kuhusiana, wataalamu wa sayansi ya jamii wanasema
mwanadamu ni kiumbe aliyeumbwa kuishi kijamii yaani kwa mahusiano na wengine, furaha ya mwanadamu
inakamilishwa kwa uhusiano kati yake na MUNGU muumbaji,uhusiano kati yake na wanadamu
wengine na uhusiano wake na vitu vilivyo mali ya MUNGU, hakuna furaha ndani ya
mwanadamu asipofungamana ama kuhusiana na MUNGU muumbaji, wanadamu wenzake na
vitu vingine alivyoviumba MUNGU.
Kabla ya dhambi kulikuwa na uhusiano mzuri na
sahihi kati ya Adamu na Hawa na muumbaji wao, waliongea naye uso kwa uso kama
rafiki yao waliishi na viumbe vyote katika bustani kwa furaha wakicheza na
simba, dubu, nyoka lakini pia wao kwa wao walijawa na furaha na amani tele kila
wakati.
Baada ya dhambi hali ya mambo ilibadilika MUNGU
hakuongea nao tena uso kwa uso, wanyama na viumbe vingine vikawa adui zao na maisha
yao yakajawa na huzuni na simanzi tele.
Hata hivyo, kwa kuwa MUNGU ni mwenye upendo
alianzisha na kumfundisha Mwanadamu kanuni za msingi za mahusiano ambazo
zikipokelewa na kufanyiwa kazi zitaleta furaha na ustawi bora kwake.
A: KANUNI KUU ZA UHUSIANO SAHIHI
1.
Utii kwa
sheria na maagizo ya Mungu; uhusiano unaendeshwa katika
misingi ya utii kwa neno la mungu na sheria yake, ndio uletao furaha, bali
uhusiano uliojegwa katika kuridhishana na kufurahishana kwa kitambo, huku amri
takatifu na maelekezo ya neno la mungu yakivunjwa, huishia kwenye huzuni na
hata kuvunjika, “mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi bali mkikataa
na kuasi mtaangamia kwa upanga’’ Isaya 1:20, “mitume na ndugu wakasema imetupasa kumtii MUNGU kuliko wanadamu” (matendo 5:29) kwa ujumla uhusiano wowote unaomuondoa
MUNGU ili kuimarisha uhusiano kati ya mwanadamu na mwanadamu au mwanadamu na
mali hauzai matunda ni sawa na mti uliokatwa na kuchimbiwa katika udongo usio
na maji, utaonekana na majani mabichi kwa kitambo tu kisha utanyauka.
2.
Upendo wa
kweli; Bwana
yesu alithibitisha kanuni hii ya uhusiano aliposema, “mpende MUNGU wako kwa moyo wako wote na kwa
roho yako yote na kwa akili zako zote, hii ndiyo amri ya kwanza iliyo kuu, na ya
pili yafanana nayo, mpende jirani yako kama nafsi yako: (mathayo 22:27-30)
angalia pia (Luka 10:27), upendo wa kweli ndiyo gundi ya
uhusiano wa aina yoyote, uwe ni urafiki, uchumba, ndoa, kazini, nyumbani na
sehemu yoyote. Upendo huambatana na matendo yote mema yanayoimarisha uhusiano
kama adabu, uvumilivu, utu wema, fadhili, kuaminiana, kuthaminiana n.k na kuondoa
matendo yote mabaya yana haribu uhusiano kama majivuno, husuda, kuhesabu
mabaya, kutokuheshimiana, kutokuthaminiana n.k (1 kor 13:1-10).
B: AINA ZA MAHUSIANO:
Kuna aina nyingi za uhusiano au mfungamano katika
jamii, baadhi ya mifano yake ni; urafiki, undugu, uchumba, ndoa na kadhalika. Mifungamano
au mahusiano haya yaweza kuwa kazini, nyumbani, chuoni, kanisani na mahali
pengine panapokutanisha watu pamoja (social agent). Aina zote hizi za mahusiano zitadumu na kumletea
mwanadamu furaha ya kweli ikiwa zitazingatia kanuni kuu mbili za uhusiano wa
ukweli yaani utii kwa sheria na maagizo ya MUNGUna upendo wa kweli.
Katika aina zote za uhusiano, uchumba na ndoa ndizo zenye changamoto nyingi na na
wengi wamekosea katika Nyanja hii, hivyo badala ya kupata furaha kama
walivyokusudia wameishia kwenye majuto, simanzi na huzuni maisha yote. Hebu
tuangalie baadhi ya ushauri wa neno la MUNGU katika aina hizi za uhusiano.
I: UCHUMBA:
Uchumba ni uhusiano halali na unaoungwa mkono na
biblia ikiwa utafanyika kama neno la MUNGU linavyoelekeza. Biblia inasema “Mwezi wa sita malaika Gabrieli alitumwa na
MUNGU kwenda mpaka mji wa Galilaya jina lake Nazareti kwa mwanamwali Bikira
aliyekuwa ameposwa na mtu jina lake Yusufu, wa mbali ya Daudi na jina lake
Bikira huyo ni Mariamu”.
Hivyo utaratibu wa kuposana au kuchumbiana umekuwepo
hata nyakati za biblia miongoni mwa wakristo waaminifu kama Yusufu na Marium
soma pia mathayo 1:18.
Kanuni ya kanisa inasema uchumba ni kipindi cha
maandalizi kwa vijan waliopendana kuoana. (soma kanuni ya kanisa sura ya 13 uchumba na ndoa).
Kwa hiyo kama kanuni za neno la MUNGU zikifuatwa
uchumba ni uhusiano mzuri uliokusaidiwa kuwaletea furaha wahusika katika
kipindi chote cha uchumba na katika maisha yao ya ndoa, kinyume chake kanuni za
neno la MUNGU zinapokiukwa wahusika hujiletea huzuni na majonzi wakati huo wa uchumba
na katika maisha yote ya ndoa ikiwa wanafanikiwa kuonana, na kuukosa uzime wa
milele kama wahusika wasipogeuka na kurudi kwa mwokozi yesu kristo kwa msaada.
Ili kijana aweze kupata furaha na heshima
maishani yapo mambo 10 ya kuzingatia katika uhusiano wa uchumba.
MAMBO 10 YA KUZINGATIA KATIKA
UHUSIANO WA UCHUMBA.
I:USIHARAKISHE.
Usiharakishe na kukurupuka kutafuta mchumba kabla
ya wakati muafaka.Pengine unaweza kujiuliza ni wakati upi ni muafaka kutafuta au
kuwa na mchumba?ni wakati unapokuwa umekomaa kiroho, kiakili na kimwili
umejitambua kikamilifu ulikotoka, mahali ulipo na unapokwenda na umetathimini
kwa makini mipango na ratiba yako ya sasa na ya baadaye ndipo waweza kuchukua
hatua hii mhimu katika maisha.
Wengi wamepuuzia hili na kukurupuka kutafuta
mchumba bila kujitathmini na kuishia kwenye uasherati na usaliti vilivyowaletea
huzuni na majuto badala ya furaha na ndoa takatifu. Biblia inasema “Ni nani katika ninyi Kama
akitaka kujenga mnara asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama kwamba anavyo vya
kumalizia asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi watu wote waonao
wakaanza kumdhihaki…….” (Luka 14:28-30).
II: USITAFUTE MCHUMBA KWA MSUKUMO KUTOKA NJE.
Usitafute mchumba Kwa kuangalizia, kushawishiwa,
kuiga au kusukumwa na ndugu, marafiki au washiriki wenzako, suala la kutafuta
mchumba linapaswa kutoka ndani yako baada ya kujithamini na kuona kuwa ni
wakati mwafaka na kupata sababu za msingi za kupata mchumba hatimaye kufunga
ndoa.
III: USITAFUTIWE MCHUMBA.
Vijana wa kiume na wa kike wanatakiwa kuwa makini
sana katika suala hili, yakupasa uwe na orodha yako ya sifa unazozitaka, cha
msingi zisipingane na neno la MUNGU, hizo zitakuongoza katika kutafuta mke au
mme utayempenda na kumfurahia, fanya maamuzi ambayo hutakuwa na sababu ya
kumfurahia mwingine.
Ushauri wa ndugu, jamaa, marafiki na viongozi wa
kanisa unafaa kuzingatiwa kwa makini,lakini maamuzi ya mwisho yatoke kwa mhusika
ambaye ataambatana na huyo mwenzi maisha yote, wengi wametafutiwa na kuishia
kulaumu na kuvunja uchumba na hata ndoa.
IV: USIFANYE UCHUMBA WA SIRI.
Uhusiano kati ya kijana wa kiume na wa kike
waliopendana, waliokubalian kuoana huitwa uchumba baada ya vijana hao
waliokubaliana kuwajulisha wazazi wa pande zote mbili na ikibidi viongozi wa
kanisa. Kuendesha mahusiano ya siri siri kunafananishwa na Nabii sawa na dhambi
ya wizi, kuiba upendo wa msichana, kwa kweli kitendo hiki hakikubaliki kabisa
na si chema kwa binti mwenyewe, kwa wazazi na hata mbele za MUNGU(soma kuchagua mchumba uk 23, soma pia Nusuru ndoa yako uk 107
“mvulana ampendaye msichana …. Bila kujulikan kwa wazazi wa msichana hafanyi
tendo jema kwa msichana mwenyewe wala kwa wazazi wake. Kwa kweli hata hafanyi
kitendo chema cha kikristo (kuchagua mchumba uk 23) madhara
ya uchumba wa siri ni pamoja na kuvunja uhusiano wenu na MUNGU, kukosa ushauri
wa wazazi na viongozi wacha MUNGU, kufasiriwa vibaya na watu wanaowaona na
kujiingiza katika vitendo viovu vya uasherati kwa urahisi. Hivyo mara baada ya
kukubaliana, ni muhimu kutoa taarifa kwa wazazi na uongozi wa kanisa.
V:USIWE NA WACHUMBA WENGI.
“Ajifanyiae rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe……..” (Mithali
18:24).
Utafiti unaonyesha kuwa vijana wengi wa kiume na wa kike wakristo huwa na
wachumba wengi kwasababu kwa sababu zifuatazo, kwanza kutokuwa na uhakika kuwa yupi
mchumba wa kweli, pili ni kutaka kupata umaarufu, tatu ni tamaa na nne ni
kutaka vya bure na tano ni kukurupuka. Hiyo siyo tabia njema kwa kijana mkristo,
kuwa na wachumba wengi kuna madhara makubwa. mfano kuwa mdanganyifu ili
kuwaridhisha wote, kusababisha ugomvi na hata kuuana miongoni mwa wa wapenzi
wako, wakigundua wote waweza kukuacha, lakini pia ni kuwapotezea muda wengine.Mungu
hapendezwi na mwenendo huo hata kidogo,uovu
huu usipoachwa, utajitokeza tena katika maisha ya ndoa baada ya harusi
(kuchagua mwenzi uk 23) muombe MUNGU kwa imani uwe naye mmoja tu kwa wakati na
inaposhindikana, tulia mwombe MUNGU naye atatuongoza mahali sahihi.
VI: USIOMBE UCHUMBA KWA MAJARIBIO “KUUDHIHAKI MOYO”
‘Kudhihaki
ni kosa ambalo halina upungufu wowote machoni pa MUNGU mtakatifu. Ingawa ni
hivyo wengi huonyesha wasichana mapenzi na kuamsha upendo wao na baadaye
wakaenda zao bila kujali Waliyonena na bila kufikiri maneno yao yatakuwa na
matokea gani kwa yule msichana. Wanapokuwa wakitangatanga huko na huko huona
sura mpya…. Na kuamsha mapenzi ya msichana mwingine hali kadhalika wakaenda na
kumsahau pia. Vile vile wako wasichana wenye mienendo kama hiyo (kuchagua mwenzi uk 23) huu ni ouvu mbele za MUNGU, wengi wamejinyonga
na kunywa sumu kwa sababu ya dhihaka za vijana ambao hawakua na dhamira ya
dhati, waliotamka nakupenda kwa
majaribio au kwa lugha inayotumiwa na
vijana kujipima uzito, kisha wakaenda zao. Hebu kijana usiombe uchumba ikiwa
huja dhamiria, wala usiombe uchumba bila kupenda au kwa kumsaidia msichana ama
kumkubali kijana kwa kumsaidia au kwa majaribio, hiki si kitendo chema kabisa
kwa anayetendewa na mbele za MUNGU.
VII: USIWE MWONGO, MUELEZE UKWELI WOTE KUHUSU WEWE.
“Nao ulimi ni moto,
ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi umewekwa katika viungo vyetu na ndio uutiao
mwili wote unajisi; huuwasha moto mfululizo wa umbile nao huwashwa moto wa
jehanamu” (Yakobo 3:6) kama kuna kitu kinachoweza kuteketeza uchumba wako ni uongo na
usengenyaji. Vijana wengi hutafuta mchumba kwa uongo kwa kujipatia sifa au
hadhi zisizo za kweli na kuficha baadhi ya mambo mhimu yanayowahusu, uwe wazi
kwa mchumba wako au kijana anayetarajia awe mchumba wako.Ikiwa una mtoto au
ulishawahi kuoa au kuolewa.Mueleze mipango au njozi zako za baadaye ili
anapofanya maamuzi ya kuwa na wewe awe ameridhika na awe tayari kuwa na wewe
jinsi ulivyo, huu ndio msingi wa upendo wa kweli.
VIII: EPUKA VITENDO VINAVYOWEZA KUTAFSIRIWA VIBAYA
Biblia
inasema “sisi ni barua
iliyoandikwa na kusomwa na watu wote”(2kor 3:2-3), kwa kuwa sisi
ni barua ya MUNGU kwa watu wanao
tuzunguka imetupasa kuepuka vitendo vyote vinavyoweza kutufanya tusomeke
vibaya.Miongoni mwa vitendo hivyo ni kukaa mazingira ya kificho mfano
gizani,chumbani au vichakani, watu wakiwaona wanawatafsiri vibaya na hivyo
kuwazuia kumuona kristo katika maisha yenu,pamoja na hayo mazoea haya ndio chanzo kikubwa kuelekea
katika uzinzi na uasherati .Kitendo kingine ni kuwa pamoja kila wakati ,ninyi
sio mume na mke,huu sio wakati wake, kitendo hiki husababisha vijana kuzama
katika mapenzi mazito kabla ya wakati,na hivyo huwa vipofu wa mapenzi,hiki
nacho ni kichocheo kikubwa cha ngono kabla ya ndoa,kitendo kingine ni maongezi
usiku wa manane, tabia hii haimpendezi mungu,saa za usiku ni saa za
kumpumzika,kukesha usiku kucha kwa ajili ya maongezi kunadhuru afya yenu
vilevile,madhara yake ni pamoja na kudhoofu ubongo,uchovu mwingi na hivyo
kufanya hata ufanisi wa kazi zako upungue,pia kitendo hiki huamsha tama za
mwili na mwisho kutumbukia katika zinaa na uasherati,na ukiwa unazungumza
chumbani unakera wengine na wanakutafsiri vibaya.Tabia nyingine ni kutumia pesa au zawadi nyingi ili kuimarisha
uchumba au kupata mchumba,kitendo hiki pia si mpango wa MUNGU,uchumba unapaswa
kujengwa katika msingi wa upendo wa kweli na si vitu.Tabia hii husababisha
upofu wa mapenzi hivyo mambo muhimu hupuuzwa na wengi hujitumbukiza katika
uhusiano wa ndoa na watu wasiofaa.
IX: EPUKA ZINAA NA UASHERATI.
“Azinie na mwanamke hana akili kabisha (Mithali 6:32), Vijana
wengi hudhani ngono kabla ya ndoa ni
ujanja na huimarisha uhusiano wao.Lakini hiki ni kitendo kinacho haribu kabisha
uhusiano wako na mwenzi wako na uhusiano wenu na mungu.Aidha uzinzi na
uasherati unamadhara na hasara zake hasa kwa wasichana.Baadhi ya hasara
wazipatazo wasichana ni kama zifuatazo:
Kupata mimba nje ya ndoa (mimba sizizotarajiawa),
kukakataliwa na wachumba wao,kuharibu uwezakano wa kupata mchumbamwingine tena,vifo
kwa sababu ya kujaribu kutoa mimba walizo pata bila ya kutegemea,kupoteza
heshima katika jamii,kuvunja uhusiano wao na MUNGU n.k Sasa kwa nini usiepuke
mambo haya kwa kuwa mwaminifu?
X: USICHUMBIE MTU WA IMANI TOFAUTI NA WEWE.
“Msifungiwe nira na wasioamini
kwa jinsi isivyo kawaida” (2 kor 6:14), kuonana na kijana mwenye
imani tofauti na wewe kunaleta migogoro mizito na isiyokoma katika maisha ya
ndoa.Mungu amezuia jambo hili tangu zamani ,akawaelekeza waisraeli taifa lake
teule wakati ule alisema “wale msioane nao, binti yako usimpe mwanawe mume, wala msimtwalie
mwanao mume binti yake (kumb 7:2,3).Sababu yake Mungu anasema “kwa kuwa atamkengeusha mwanao
asimfuate Mungu ili wapata kuabudu miungu mingine(kumb 7:4) Vijana wengi wameyapuuza maagizo haya
mema na kuongozwa na tama za mioyo yao kama ilivyokuwa kwa Samsoni(waamuzi 14:
) wengine wakidai watawaongoa , huku ni kujidanganya ,Suleimani alikuwa na
hekima kuliko watu wote wa wakati wake na wakati huu, alifanya kosa hilo hilo
akitaka kuongoa mataifa yaliyomzunguka kwa kuoa binti zao lakini mwisho
aliishia anguko kuu la kiroho na kugeukia miungu yao “Suleimani akawapenda wanawake wengi wageni
nao wakaugeuza moyo” (1fal 11:) kama Suleimani alishindwa, vipi
wewe?, anaweza kukubali ili kukuridhisha na kukupata wewe lakini kwa hakika huo
sio uongofu wa moyoni na matokeo yake utayashuhudia baadaye.Ndoa zimegeuka kuwa
mahabusu na jela ndogo,migawanyiko ya imani,malumbano yasio koma,ugomvi usio
koma, kwa sababu watu wawili wenye itikadi na falsafa mbili tofauti waliunganishwa kwa ndoa bila ya kujali mausia ya neno la
Mungu.Kijana ikiwa uliingia katika mausiano ya namna hii bila kujua au kwa
kujua kwa neema ya yesu na hekima ya mbinguni vunja uhusiano huo mara moja.
SEHEMU YA PILI: Juma Tatu –
04/06/2012.
II: NDOA.
“Ndoa na iheshimiwe watu wote na
malazi yawe safi (Ebrania 13:4) kama tulivyo tangulia kusema kanuni
kuu mbili zinazoweza kuleta furaha katika mahusiano yoyote ni kutii sheria na
maagizo ya neno la Mungu na upendo wa kweli,Furaha ya ndoa
hupatikana pale tu wanandoa watakapoamtanguliza na kumheshimu Mungu katika
maisha yao ya ndoa, kadri tunavyomkaribia Mungu ndivyo tunavyo karibiana sisi
kwa sisi, biblia inasema “Bwana asipoijenga nyumba waijengao wafanya kazi bure, na Bwana
asipoulinda mji waulindao wakesha bure (zab 127:1) ,hivyo kumtii
Mungu na upendo wa ukweli kati ya wana ndoa
na kati yao na Mungu ndizo kanuni kuu katika maisha ya ndoa kwa maelezo
yenye ufafanuzi, napenda kumnukuu mshauri mkongwe wa ndoa na mwandishi wa
kitabu cha nusuru ndoa yako.Pastor Daudi Makoye, juu ya sheria kumi za kulinda
uhusiano na mwenzi wako na kanuni kumi za ndoa.
A: SHERIA KUMI ZA KULINDA UHUSIANO NA MWENZI WAKO
i)
Chunga ulimi wako, daima sema machache kuliko unavyofikiri.
ii)
Timiza ahadi hatakama inagharimu.
iii)
Usikose nafasi ya kusema neno linalolitia moyo kwa siku.
iv)
Uvutiwe na mume au mke wako kwa yale afanyayo.
v)
Usibishane naye.
vi)
Zuia kusema ovyo kasoro za mwenzako.
vii)
Uwe mwangalifu usimkwaze mwenzako katika hisia.
viii)
Usijali maneno yanayopelekea kukuumiza.
ix)
Usimdanganye mwenzi wako.
x)
Fanya kazi, vumilia na fanya mambo yote yawe ya kupendeza.
B: KANUNI KUMI ZA NDOA.
i)
Usiwe na mke au mume mwingine ila Yule uliye funga naye ndoa.
ii)
Usijifanyie wapenzi wengine mfano wa mume au mke wako, usiwahusudu
wala kuwatumikia.
iii)
Usimtaje ovyo ovyo mume wako au mke wako kwa majirani au ndugu usije
ukadharaulika wewe na mkeo.
iv)
Ikumbuke siku ya harusi uiheshimu na kuisheherekea wewe mkeo na wanao.
v)
Waheshimu wakwe zako ipasavyo.
vi)
Usiue pendo lenu.
vii)
Usizini.
viii)
Usiibe haki ya ndoa na mali yenu.
ix)
Usimshudie uongo mume wako au mke wako.
x)
Usitamani mke au mume wa mwenzako
Haya ni baadhi ya mambo au ushauri unaoweza
kusaidia kuimarisha uchumba na ndoa zetu. Lakini jambo kubwa ni kumfanya KRISTO
awe mkuu na mwenyeji wa uchumba wetu na ndoa zetu wala tumsimfanye mgeni asiye
na uhuru au mamlaka katika uchumba wetu au ndoa zetu.
Napendekeza kwenu kitabu cha Pastor Makoye “Nusuru ndoa yako’ na Pr.Mange “It is not good’ Kuchagua mchumba cha E.G.white
Kisomwe na kila kijana na mwanandoa,ni hazina iliyositirika.
MJADALA WA MASWALI YA PAMOJA.
Mwendesha
somo awashirikishe wanadarasa kwa nafasi ya kujadili mambo yaliyozungumzwa hapo
juu kwa pamoja ili kupanua uelewa na kutiana moyo kufanya mahusiano
yaliyosahihi mbele za MUNGU.
SOMO LA TATU: MAVAZI NA MVUTO.
[ 1Timotheo 2;9,10,
1Petro 3;3-5 ].
SEHEMU
YA KWANZA.
UTANGULIZI:
Tumezungukwa
na ishara kila mahali, lugha zetu, utamaduni, jamii, siasa kila kitu kwa
kiwango Fulani hutujia vikiwa katika mfumo wa ishara; bendera, nembo, picha na
kauli mbiu, sanaa , mashairi, na taratibu za ibada hutumika kutegemeana na
mahali; hivyo vyote huwa na maana kubwa kuliko vitu vyenyewe.
USAFI WA MWILI.
Katika kutunza mwili wako ili uvutie, hautaishia
kwenye vyakula tu na kuupatia mahali pa kulala; unahitaji pia utunzaji wanje.
Suala hili la utunzaji wa mwili na usafi wa nje ni la muhimu sana hasa kwa
wasichana. Wavulana nao wanaguswa sana na usafi wa nje, ingawa ukilinganisha
kati ya wasichana na wavulana utagundua kwamba wasichana wanaguswa zaidi kuliko wavulana, na ndiyo
maana hakuna mvulana atakayevutiwa na msichana
mwenye kamasi, anayenuka mdomo, kwapa, chawa kichwani, mafuta yenye
harufu mbaya kichwani na katika marinda ya magauni yaliyopitwa na wakati.
Hali hii ya uchafu wa nje, hufanya sifa
ya tabia njema ya ndani isionekane kwa msichana au mvulana, mwonekano wa nje
ndio unaochagia msichana kuposwa na ndiyo maana siku hizi wasichana wanakazania
urembo na kusahau urembo wa tabia zao, usafi wa nje na ndani visitenganishwe na
vile vinavyoonekana kwa nje, iwe hivyo na ndani pia au vile ulivyo kwa ndani,
ionekane hivyo na nje pia.
Ukilejea katika kitabu cha Ruth 3:3,
Naomi alimwambia Ruthu “Basi
wewe oga, ujipake mafuta, ujivike mavazi yako kisha uende kwenye uga”.
Katika usafi hapa, Ruthu aliambiwa kufanya mambo matatu ambayo hata vijana wa
leo wanaambiwa kuyafanya nayo ni (a) Aoge (b) Apake mafuta (c) Avae mavazi.
Miili yetu imeumbwa kwa kuwa na viungo
vingi, lakini kuna viungo ambavyo macho ya watu yanaweza kuviona kirahisi. Vipo
viungo ambavyo vinaweza kuonekana kirahisi. Vipo pia viungo ambavyo vinaweza
kujificha lakini viungo kama; meno,
mdomo, pua, masikio, macho, nywele , miguu na vidole vya mikono havifichiki.
Viungo hivi vinaweza kukudhalilisha na kuharibu haiba usipoviweka katika
usafi wa kutosha, Na sasa tuanze kuangalia kiungo kimoja baada ya kingine.
Kama
waadventista tunaelewa lugha ya biblia inavyotumika kuwakilisha kitu fulani
v Somo
hili linalenga katika mifano ya Biblia ya namna mvuto na mwonekano wa mkristo
wa kweli waweza tambulishwa na kielelezo cha;
MAVAZI.
Mavazi ya wasichana yanasifa kuu mbili;
kwanza ni mtindo (mshono) wa mavazi, pili ni usafi wa kawaida. Hivyo mtindo wa
vazi na utunzaji wake hutazamwa sana na watu na hapo ndipo wataanza kukuweka
katika makundi Fulani Fulani kulingana na muonekano wanje.
Je, haiwapasi watu wa mungu (wakristo)
kuwa mfano wa kuigwa kwa muonekano wao wa nje na ndani? “Ni vema
kuwa kielelezo kwani katika mavazi kuna ujumbe unaowasilishwa kwa wengine”.
Leo wamevumbua mishono mbalimbali yenye ujumbe yenye ujumbe kama vile sina
adabu, simjali baba, sina kovu, wowowo na mishono mingi kama hiyo, ambayo
shetani amekuwa akiitumia kudhalilisha uumbaji wa mungu na kuyapinga maandiko
yanayosema, “uvae mavazi yanayositiri mwili” mitindo kama hii ni aibu kwa binti
mkristo kuivaa, kwa mabinti wanaovaa mavazi kama haya, wanaonekana kuwa ni
wahuni kwani inavaliwa na watu wenye sifa hiyo na hivyo hutashangaa kusikia
mabinti hao wakipigiwa miluzi huko mtaani.
Mabinti wa kikristo wanashauriwa
kuepuka mapambo mengi. Mavazi yachaguliwe kwa ajili ya uimara wake kuliko kwa
kufanya maonesho. Mavazi yetu yaoneshe uzuri wa tabia ya mtu na yawe mavazi ya
kawaida. “kufuatisha namna za walimwengu zisizo na kiasi katika mavazi ya
wanaume na wanawake kunaonesha upungufu katika kuangalia mambo ya maana, kuna
mavazi yasiyofaa na yanakiuka sheria za uadilifu, je wakristo waadventista
wasabato wanayo kila sababu ya kujilinda na sheria ya uadilifu wasiwe wavunjaji
wa maadili katika jamii.
Sababu kubwa ya kushamiri kwa ubakaji
ni uvaaji mbovu wa mabinti ambao ni wabishi, wanaojitosa katika kuvaa mavazi
hayo kama vipofu na wasiofikiri sawasawa madhara yake. Wengine huvaa mavazi ya “sina adabu” au “simjali baba” mitindo
ambayo huwafanya watembee mitaani wakionesha nguo zao za ndani jambo ambalo
huamsha tamaa za wanaume na kuchochea ubakaji wa wanawake.
Mabinti wasio waungwana, huvaa mavazi
yao na kuonesha nguo zao za ndani. Kwa binti je, anayosababu gani ya
kuwafanya waoneshe nguo zao za ndani? kwani wao ni maduka?. Wengine
wanavaa mitindo iitwayo “sina kovu” uvaaji huu ni wa kuhamasisha mazingira ya
kupendwa ili waolewe. Badala yake wanaboresha mazingira ya zinaa na kubakwa.
Ingekuwa kheri kwa wote wanaosikia ujumbe huu kubadili mitazamo yao mibaya ya
kupenda mavazi hayo yasiyofaa wakristo tuwaachie watu wa ulimwengu wasio na
nuru hii lakini sisi tuliopewa mwanga huu kwa neema ya yesu tubadilike tusaidie
na wengine.
Miongoni mwa ujumbe tunaopata kutokana
na mavazi ni kumtambua mtu kama “kahaba” Mwanzo 38: 14-16 “huyo tamari akapewa habari, kusema
mkweo anakwenda timna, akate manyoya ya kondoo wake. Basi akavua nguo za
ujana wake, akajivika utaji, akajifunika uso, akakaa mlangoni pa Enaimu,
karibu na njia ya kwenda timna, maana aliona kwamba shela amekuwa mtu mzima
wala hakuozwa awe mkewe” “yuda alipomwona alimdhania kuwa ni kahaba, maana alikuwa amejifunika
uso (nguo za kikahaba) Mithali 7: 10-11. Akamgeukia kando ya njia, akasema
niruhusu niingie kwako. Maana hakujua ya kuwa ni mkwewe”. Hivyo
tunaona mavazi ya kikahaba na mavazi ya kijana yalitambuliwa hata katika vizazi
vilivyopita. Hivyo basi kuna mavazi ambayo binti akiyavaa yanaweza kumweka
katika kundi la watu wa aina fulani na kufanya ajulikane kuwa ni mtu wa namna
fulani. Pia yaweza kuongeza au kupunguza sifa ya binti.
Kwa ujumla tunaona kuwa makahaba
walikuwa wakijulikana kwa mavazi yao. Mithali 7: 10-11. Je wewe mavazi yako
yanayokufanya ujulikane kama nani ? Angalia sana mavazi yako yasije yakaharibu
sifa yako njema. Mavazi yasiyofaa yanaharibu sifa njema ya mtu..
Naam
japokuwa sisi siyo kile tunachovaa, kile tunachovaa kinaweza kueleza mengi
kuhusu vile tulivyo; Kwa mantiki hiyo kama ilivyo kwa mifano yote, mavazi
yanaweza kuwakilisha kitu kikubwa kuliko mavazi yenyewe, katika mavazi kama
yalivyo mambo mengine tumejaliwa kumtukuza muumba wetu kwa usafi na yenye
kukidhi afya yetu tena mazuri naya kufaa pia.
KANUNI
YA MAVAZI:
Twafahamu
tabia ya mtu kwa namna ya mavazi anayovaa.Mwanamke mwenye adabu, Mcha Mungu
atavaa kwa adabu. Akili nzuri, moyo wa uadilifu, utadhihirishwa kwa kuchagua
mavazi yanayofaa na yasiyo na mapambo mengi.Mtu asiye na kiburi katika mavazi
yake na hali yake huonyesha kuwa mwanamke wa kweli huainishwa kwa uadilifu.
Nabii anasema; “Nawasihi watu wetu kuenenda kwa uangalifu na kwa tahadhari
mbele za Mungu.Hebu dada zetu wavae pasipo urembo, kama wengi wafanyavyo,
wakiwa na mavazi mazuri ya vitambaa vidumuvyo, ya kufaa siku hizi; Tena mavazi
yasiwe jambo kubwa mawazoni. Yawapasa wajivike nguo za adabu, kusitiri aibu ya
uchi na kuwa na kiasi. Wapeni walimwengu kielelezo cha nguvu cha
kujipamba kwa neema ya Mungu. Wakristo wangemwiga kristo na kufanya uvaaji wao
kupatana na neno la Mungu. Kwa
unyenyekevu wangefuata unyofu, wasijali sifa, za kitambo na yafaa washikilie
kutenda mema kwa sababu ya uzuri wa wema wao” Kutayarisha njia 1 (onyo juu ya
mavazi UK.34.)
MAFUNDISHO
YA BIBLIA. [ 1Timotheo 2;9,10, 1Petro 3;3-5 ]
v Kristo
aliona upendo wa mavazi, nae alionya, naam, akaamuru wafuasi wake wasiyafikiri
sana hayo. “Na mavazi ya nini kuyasumbukia”usijisumbue kwa wakati wote kwa
kujaribu kuiga namna zote za mavazi
zisizo na maana.vaa nguo safi na nzuri, lakini usijionyeshe ama kwa kuvaa
maridadi, ama kwa kuvaa vibaya kwa uzembe. Tenda kana kwamba unajua kuwa jicho
la mbingu linakutazama, na ya kuwa unaishi chini ya kibali cha Mungu ama
kinyume na mapenzi yake.
Nabii anasema; “nalielekezwa
kwenye mafungu hayo juu” kiburi na upotevu wa mali katika
mavazi ni dhambi ambayo mwanamke hupenda hasa. kiasi katika kuvaa ni
wajibu wetu wa kikiristo, kuvaa bila kujipamba, kuepukana na mavazi ya kubana, yasiyo na utukufu,
yasiyo mafupi yanayodharirisha hekalu la Roho Mtakatifu kuwa kiwanda cha mvuto
katika kutenda dhambi. Ni jambo linalopatana na IMANI YETU. Kutayarisha njia 1
(onyo juu ya mavazi)
KUCHUCHUMILIA VAZI LA
KRISTO LILILO BORA ZAIDI.
v Kiini
safi cha upendo kitaipanua roho ya mtu ili kutoa nafasi kwa mambo bora zaidi
kwa kutamani kuwa kama kristo na kutamani vazi la neema ya kristo yaani tabia
yake na kuwa na mtindo wa maisha unaomtangaza kristo kama Bwana na Mwokozi wao
kwa kupitia namna wanavyovaa.
Hatari
kubwa ni kuwa wengi wanaojiita wakristo hawajui nguvu za roho ambazo wangeweza
kupata kama wangetoa habari ya Ufalme wa Mungu kwa kupitia mavazi yao na
kuonesha kielelezo cha kuwa Wana na Binti katika Ikulu ya Mfalme waliotayari
kusimama katika Ikulu ya Mbinguni kwa namna wanavyovaa. Lakini jamii ya
wakristo wengi wameridhika na hali ya kudumaa kiroho kwani wamejaribu Kutafuta
kumtangaza shetani, dunia na mivuto na anasa zake kuwa bora zaidi kuliko
Kristo, Mbingu na uzuri wake ambayo kristo ametuandalia na hili hudhihirishwa
na maisha ya wakristo wengi.
v Ndugu
msidanganyike, mungu hadhihakiwi. Utakatifu tu, wala si kitu kingine, ndio
utakaotufanya kuwa tayari kwenda mbinguni. Unyofu na Uchaji wa hakika katika
mambo ya maisha ndio uwezo pekee wa kuwapa tabia safi, bora na kuwawezesha
kuingia mbele za Mungu akaae penye nuru isiyoweza kukaribiwa.
Wanaume
na wanawake walidhikao na tabia ya kudumaa na
kulemaa kiroho hawawezi kuingia mbinguni ikiwa hawezi kufanya Uamsho na
Matengenezo haraka iwezekanavyo kwa kuacha mavazi yasiyomtangaza kristo. Tabia
ya mbinguni lazima ipatikane hapa duniani ama sivyo haitapatikana kamwe na
wengi tutapotea si kwa sababu hatupendi kwenda mbinguni bali tulipuuzia ujumbe
wa wokovu na kuzidisha kiburi kwa mambo matakatifu.
MVUTO WA NAMNA YA MAVAZI.
v Kupenda
mavazi huhatarishatabia za uadilifu na kumfanya mwanamke kuwa kinyume cha mke
mkristo mwenye adabu nay a kiasi. Mavazi ya kujionyesha, ya bei kubwa, mara
nyingi huzidisha tamaa kwa mvaaji na kuamsha tama mbaya moyono mwa mtazamaji.
Mungu anaona kuwa uharibifu wa tabia hutanguliwa na kuendekeza kiburi na
umaridadi usio na maana.
v Wengi
wetu tumesahau kuwa Mungu ametuita kuwa mfano wa kurejesha sura yake iliyopotea baada ya dhambi kuingia
ni huzuni kubwa pale tunapovaa kama walimwengu wasioamini na kuongolewa na
ulimwengu
v Vijana
wapendwa nia tuliyo nayo ya kuvaa kama mtindo wa siku hizi, watu wenye akili
watahesabu jitihada zetu za mapambo ya nje kuwa ni Thibitisho la nia dhaifu
tuliyo nayo na mioyo ya kiburi.
v Kuna
vazi ambalo kila mtoto na kijana anaweza kulitafuta na kulipata tu pasipokuwa
na hatia. Hilo ni Haki ya Watakatifu, ikiwa tungekubali tu kufanya bidii
kulipata vazi hilo kama tunavyojitahidi katika mitindo ya mavazi yetu kwa kuiga
ulimwengu, Haingepita mda mrefu tungevikwa haki ya kristo na majina yetu
hayangefutwa katika kitabu cha uzima.
v Wakati
mavazi ya dunia huchakaa mavazi bora ya Mungu huleta furaha, sifa na wokovu wa
milele, hata hivyo lazima tuvae vazi la Mungu la wokovu ili tuweze kupata
mibaraka anayoitoa.
v Zekaria
3:4. Kuhani mkuu Yoshua anajikuta katiak mahakama ya hukumu akiwa na mavazi
machafuakishitakiwa kwa dhambi zake zote. Hakimu wake, badala ya kumhukumu,
anamvua mavazi achafu na kumvika mavazi safi na kumwita kuwa mtii.
v Ikiwa
kweli ujmbe wa Uamsho na Matengenezo umepokelewa na kristo kupokelewa katika
mioyo ya watu kwa njia ya Roho Mtakatifu Uongofu wa kila kitu kisichopatana na
Neno la Mungu kitaachwa. Lakini kama sivyo sauti hii itakuwa kama ukataji wa
matawi {jambo ambalo si ufumbuzi wa kudumu kwani yatachipua tena} na kuzidi
kutuvuta katika giza kuu.
v Shetani
nafurahia kuwavuta wengi kuwa tayari kwa pambano dhidi ya kristo kwa wengi kuwa
tayari kupingana na mwonekano wa kristo katika dunia hii na hatari kuu
inayoonekana kwa macho ya kiroho ni pambano hili kuwa sehemu ya kanisa leo ili
Mlango wa Rehema ufungwe wakiwa na malumbano na kuacha kujiandaa kwa ujio wa
kristo.
v Mungu
aliyewavika Adamu vazi la Utukufu alitegemea mwanadamu kuwa leo katika hali ya
kuonyesha Utukufu wa Mungu hata kwa namna ya mavazi yake lakini kutokuwa na
hofu ya Mungu Mwanadamu ametenda atakavyo kwa kufuata njia za ibilisi hivyo
kuifanya Dhambi kuwa na Mvuto kuliko Utakaso.
v Angalizo;
wengi wamedanganywa na hali yao ya mioyo na kunukuu vifungu vya biblia kuwa
kinga ya wao kutenda dhambi, hiyo ni dhambi kubwa sana kwani ni ya makusudi na
inatumia vibaya maandiko Matakatifu. Ati Mungu haangalii nje( mavazi) isipokuwa
mioyo kauli hii iko ndani ya biblia na shetani amewavuta wengi katika nyavu
zake kwa nukuu hii na imekuwa tabia yake hata wakati wa yesu alisomewa kifungu
cha biblia; Jibu ni kweli Mungu huangalia ndani ya moyo lakini Mungu akiwa
ndani ya moyo Huwezi kuvaa mavazi yanayomtangaza vibaya Kristo.
SEHEMU
YA PILI.
SOMO: UTUNZAJI WA NYWELE.
Mungu alipomuumba mwanadamu alimaliza
kila kitu na akaona ya kuwa ni chema sana, mungu alimwagiza mwanadamu kutunza
kile alichopewa. Biblia inasema; lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni
fahari kwake. Kwa sababu amepewa zile nywele ndefu ili ziwe badala ya
mavazi “(1kor. 11:15)”. Katika (1kor.
11:3), Biblia inasema, “lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanaume ni
kristo na kichwa cha mwanamke ni mwanaume na kichwa cha kristo ni mungu” .
Unapomtazama mwanamume kichwani
inatakiwa taswira ya kristo ndiyo ionekane, ukimtazama mwanamke taswira ya mwanamume ionekane kwake na utakapo mtazama kristo
amuone mungu kichwani pake. (1 Kor.11:4), mwanamume hapaswi kufunika kichwa
chake anaposali au kuhutubu maana anaaibisha kichwa chake “kila
mwanamume asalipo au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa, yuaiibisha kichwa
chake”. Anaaibisha kichwa
kwasababu atakuwa amemfunika kristo ambaye anatakiwa kuonekana, ndiyo maana
wanaume hawafuniki vichwa vyao hata kwa kuvaa kofia wanapokuwa kanisani au
wasalipo maana kristo anapaswa kuonekana, utazamapo kichwa cha mwanaume.
Jambo hili ni tafauti kwa wanawake, (1 Kor.11:5) “bali kila mwanamke asalipo au anapohutubu,
bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake kwa maana ni sawasawa na Yule
aliyenyolewa”. Hapo maandiko yanaonesha kuwa, kwa mwanamke
kufunika kichwa ni jambo sahihi na ndiyo maana hata leo katika makanisa yetu,
tunashuhudia wakina mama wengi wao huingia kwenye ibada wakiwa wamefunika
vichwa vyao kwa vitambaa lakini kwanini wamekuwepo ambao hawajafunika kwa
vitambaa? Biblia inasema “…bila kufunika
kichwa yuaaibisha kichwa chake, kwa maana ni sawasawa na Yule aliyenyolewa”
kumbe mwanamke akisali bila kufunika
kichwa ni sawa na Yule ambaye hajanyolewa ndipo anapaswa kufunika
kichwa chake. Sasa tunatambua kwamba ambaye hajanyolewa ndipo anapaswa kufunika
kichwa chake, sasa tunatambua kwamba ambaye hajanyolewa ni sawa kabisa na Yule
ambaye amefunika kichwa, lakini asiyefunika kichwa ni sawa na aliyenyolewa.
Kumbe nywele za mwanamke zinafunika kichwa chake sawa na yule aliyefunika kwa
kitambaa. Hivyo tunaona si vyema kwa mwanamke kunyoa nywele zake maana
zinahitajika ili zifunike kichwa chake ili mume wake aonekane, na kwa kuonekana
kwa mwanamume kwenye kichwa cha mwanamke, kristo anaonekana, maana yeye
hutawala au kumiliki kichwa cha
mwanamume, kupitia kwa kristo mungu huonekana.
Paulo aliwaambia wakorintho (1 kar 11:6), “maana mwanamke asipofunikwa na akatwe
nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe”
kauli ya Paulo ya kuwambia wakorintho “…mwanamke
asipofunikwa na akatwe nywele” alisema hivyo huku akitambua kuwa
kukatwa nywele katika jamii hiyo ni aibu hata wao wanafahamu, sasa ikiwa agizo
la kufunika haliwezekani bora wakate jambo ambalo kwao haliwezekani kabisa,
sasa kama kwao haliwezekani maana ni aibu ndipo Paulo anamalizia kwa kusema “….Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele
zake au kunyolewa na afunikwe”
hii ilikuwa na namna ya kuendelea kusisitiza ufunikwaji wa nywele kwa
wanawake maana hakuna njia nyingine.
Sababu zinazomfanya mwanamume asifunikwe
kichwa na mwanamke kufunikwa kichwa zinaelewa wazi kuanzia (1 kor
11:7-10) mwanamume, haimpasi kufunikwa kichwa maana yeye ni mfano wa utukufu wa
mungu, hivyo akifunikwa kichwa ni sawa na kuufunika utukufu wa mungu. Lakini
mwanamke imempasa afunikwe kichwa ili utukufu wa mwanamume uonekana na huo
ukionekana unamfunua kristo ambaye kupitia kwake utukufu wa mungu ndio
unaoonekana (1 kor 11: 7-9).
Mwanamke anapofunikwa kichwa, anaonesha
dalili ya kumilikiwa kichwani, si kwa ajili ya mwanaume tu bali kwa ajili ya
malaika. Mtumishi wa mungu Paulo anauliza maswali ambayo majibu yake
yanatupatia msimamo wa nini cha kufanya, Paulo anauliza, je! Inapendeza
mwanamke amwombe Mungu asipofunikwa kichwa?, (1 kor 11:13). Jibu la swali hilo
linapatikana katika (1 kor 11:5, 10). “Bali kila
mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa chake; kwa maana ni sawa
sawa na yule aliyenyolewa”
kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani, kwa ajili ya
Malaika.
Je! Mwanamuke naye anapaswa kuwa na
nywele ndefu kama mwanaume? Mtumishi wa mungu Paulo anasema katika (1 kor 11:14), “je! Hayo maumbile yenyewe hayawafundishi ya
kwamba mwanake akiwa na nywele ndefu ni fahari kwake?, Kwasababu amepewa zile
nywele ndefu ili ziwe badala ya mavazi”.
Wanawake wanapaswa kuwa na nywele ndefu maana ni fahari kwao. Hapa Bibilia
inaonesha kuwa haina ugomvi na mwanamke anayekuwa na nywele ndefu alizopewa na
Mungu ili ziwe badala ya mavazi yaani mavazi ya kufunika kichwani. Hivyo mwenye
nywele ndefu ni sawa tu na yule aliye na mavazi ya kufunikia kichwani. Mungu
amewapatia wanawake nywele ndefu ili ziwaongezee fahari, sasa kama nywele hizo
umepewa na Mungu, unapaswa kuzitunza. Hapa Bibilia inazungumzia nywele ambazo
mwanamke amepewa na Mungu, wala Bibilia haijataja wala hajamaanisha nywele za
bandia. Fungu linasema “lakini mwanamke
akiwa na nywele ndefu ni fahari kwake, kwa sababu amepewa zile nywele ndefu
ili ziwe badala ya mavazi (1 kor 11:15)”. Jiulize swali hili, je, nywele
ulizo nazo umepewa na Mungu au umepewa na wachina (wazungu).
MWENDELEZO WA SEHEMU YA
TATU
.
SOMO:
NI KUPAMBA? AU NI KUTUNZA NYWELE.
Wanawake wanashindwa kutofautisha kati
ya “kutunza nywele” na “kupamba nywele “lazima
utofautishe kati ya kutunza na kupamba.
Kamusi ya Kiswahili sanifu inatoa maana
ya maneno haya:
“Kutunza” maana yake ni kukiweka kitu katika hali
nzuri ili kisiharibike.
“Kupamba” maana yake ni kuweka urembo au nakshi zaidi
ya kawaida yake.
Wasichana wengi na wanawake kwa ujumla
katika ulimwengu huu wa leo wameamua kupamba nywele zao badala ya kuzitunza.
Kupamba nywele kunaweza kuwa na hasara
kadha wa kadha ambazo huambatana na matumizi ya vitu vitumikavyo kupambia
nywele hizo. Hasara hizo ni za kiuchumi na kiafya lakini hasara nyingine kubwa
ni hasara ya kiroho.
(a) Madhara
ya Kiuchumi.
i.
Gharama
kubwa katika kupamba nywele. Wanawake wengi wanatumia pesa nyingi kununua mapambo ya
nywele, kwenda saluni, na kuwalipa mafundi wa kuzilemba na kuzipamba. Wanadhani
kwa kufanya hivyo watapendeza na kuongeza kukubalika kwao, kumbe wanajiweka
katika sehemu mbaya mno. Wavulana wazuri japo hawawaambii waziwazi, wanawaogopa
wasichana hao kwa sababu wamejiweka katika daraja la watu wa gharama kubwa.
Vijana hao wa kiume huwa wanawakwepa kwa kuhofia gharama za kupamba nywele za
mwanamke huyo.
ii.
Kupamba
nywele kunahitaji muda wa kutosha ili kuzishughulikia. Muda mwingi ambao ungeweza kutumika
kwa shughuli nyingine za kimaendeleo, unapotezwa kenye upambaji wa nywele. Kama
muda huo ungelitumika kuzalisha au kufanya kazi fuluni ya kiuchumi basi
wanawake hao wangepunguza gharama kubwa za maisha na kuongeza uzalishaji kwa
matumizi mazuri ya muda.
(b) Madhara ya kiafya:
MADHARA
YA KIAFYA YANAYOTOKANA NA MATUMIZI YA VIPODOZI.
Mamlaka
ya madawa na chakula (marekani)
imetafsiri vipodozi kama kemikali ambazo hutumika mwilini kwa lengo la kuosha,
kuongeza uzuri na mvuto bila kuharibu kiungo cha mwili na kazi yake. Kwa lugha
rahisi vipodozi hubadilisha muonekano wa mtumiaji. Vipodozi huhusisha; kemikali
za ngozi, “lotion”, poda, marashi (perfumes), mafuta ya mdomo (lip sticks and
lip shine), rangi za kucha, kemikali za uso na macho (eye and facial make up),
rangi za nywele (hair colours), marashi ya nywele (hair spray and gels), mafuta
ya kuogea na michoro ya mwili (tattoos).
Baadhi
ya kemikali (ingredients) za vipodozi zenye madhara mwilini ni;
(i)
Rangi za kucha zina kemikali iitwayo
“sodium lauryl sulfate” ambayo husababisha ugonjwa wa ngozi (dermatitis).
(ii)
Kutumia “make up” kwa muda mrefu husababisha
ugonjwa wa nywele za kope (eyelashes), ambao humfanya mtumiaji awe na hatari ya
kupata ugonjwa wa macho (keratitis).
(iii)
Kemikali zinazotumika kutunza vipodozi
(preservatives) kama “ureas” zinasababisha ugonjwa wa ngozi (dermatitis). Aidha
kemikali zingine kama methyl, propyl na butyl zinaweza kusababisha saratani ya
matiti (breast cancer).
(iv)
Vipodozi vinavyotokana na “petrol” au
“paraffin” vinaziba vitundu
vidogo vidogo vya ngozi na kufanya
ngozi isitoe uchafu vizuri na hivyo kusababisha chunusi.
(v)
Kemikali kama “oxybenzone” na
“octylmethoxycinnamate” inaharibu mfumo wa hormone, hivyo kuathiri shughuli za
kikemikali za mwili.
(vi)
“propylene glycol” inasababisha
matatizo ya macho, saratani, inaathiri uzazi (wajawazito) na pia ni sumu endapo
mtu atakunywa kwa bahati mbaya.
(vii)
“sodium lauryl sulphate” inayowekwa
kwenye cream nyingi na shampoo inasababisha ngozi kuwasha, huingia mwilini kwa
urahisi na hukusanyika kwenye jicho, ubongo, moyo na ini kwa muda mrefu, hivyo
kuathiri utendaji wa viungo hivyo.
(viii)
Rangi za vipodozi zinasababisha saratani.
(ix)
Marashi (perfumes). Perfume (1) inaweza
kutengenezwa na kemikali hadi 200.
Baadhi ya kemikali hizo husababisha maumivu ya kichwa, kizunguzungu, chunusi,
kukohoa, ngozi kuwasha, aleji na kutapika.
(x)
Kemikali nyingi huharibu na kuondoa
seli (cells) za ngozi zilizokomaa (melanin) na kuacha seli zilizo changa; hivyo
kuathiri ulinzi ambao ngozi huutoa dhidi
ya vimelea vya magonjwa na mionzi ya jua. Kwa hali hii mwili upo hatarini
kushambuliwa na vimelea vya magonjwa, saratani ya ngozi na kuumia kwa urahisi.
Kwa ufupi; kemikali (ingredients) zifuatazo ni htari kwa afya yako; methyl, propyl,
butyl, ethyl diethanolamine (DEA) or Triethanolamine (TEA), Diazolidinyl urea,
sodium lauryl, petrolatum, synthetic colours e.t.c
Lakini pia kemikali ya Methylmercury inoyotumika kwenye vipodozi na
kemikali za kukuzia nywele ina madhara yafuatayo;
(a)
Kwa vitoto ambavyo bado viko tumboni
(fetus), watoto wachanga waliozaliwa (infants) na watoto wakubwa kidogo
(children), hupata madhara ya vipodozi hivyo kupitia mama zao wakiwa tumboni.
Madhara hayo ni pamoja na kuadhiri ukuaji wa ubongo wa mtoto na mifumo ya mwili
(effects on baby’s growing brain and nevous system).
(b)
It also affects peripheral vision and
disturbances in the body, especially sensations (hisia katika) in the hands
(mikono), feet (miguu) and around the mouth (maeneo ya midomo).
(c)
Lack of coordination movement (kuharibu
mwondoko wa mwili); impairment (madhara katika) of speech (kuogea), hearing
(kusikia), walking (kutembea) and muscle weakness (uthaifu wa misuli).
(d)
Husababisha ugonjwa wa saratani ya
shingo ya kizazi, saratani ya ngozi, saratani ya mifupa, saratani ya damu.
Ingawa ugonjwa huchukuwa muda mrefu kudhihirika.
(e)
Disturbances in sensation, (kuharibu
mifumo ya hisia ya ngozi).
(f)
Changes in never responses,(mabadiliko
katika mwitikio wa neva).
(g)
Performance deficits on tests of
cognitive function,(kuharibu uwezo wa kuelewa).
(h)
Kidney effects, (madhara ya figo)
(i)
Respiratory failure,(kuathiri mifumo ya
upumuaji).
(j)
Death,(hupelekea kifo).
(k)
Skin rashes and dermatitis, (michubuko
ya ngozi na muwasho).
(l)
Mood swings, (kubadilika kwa hali ya
mtu ovyo bila sababu)
(m)
Memory loss, (kupoteza uwezo wa
kumbukumbu).
(n)
Mental
disturbances, (kuvurugika akili).
(o)
Muscle weakness.
Walioadhirika na matatizo hayo waonane na wataalam wa Afya
kwa msaada zaidi. Makampuni mengi hayaorodheshi kemikali zote zilizotumika
kutengeneza vipodozi hususani zenye
madhara makubwa. Bidhaa nyingi zinapambwa kwa majina mazuri kama “natural”
ama “organic”
wakati zinamadhara makubwa kiafya.
TAARIFA YA WIZARA YA AFYA (2004) KATIKA HOSPITALI ZIFUATAZO:
Hospitali ya Mirembe na Taasisi
ya Saratani Ocean Road (ORCI).
Hospitali ya
Mirembe inahudumia wagonjwa wenye matatizo ya akili, wakati hospitali ya
oceanroad inhudumia wagonjwa walioathirika na magonjwa ya saratani. Kumbuka
mpendwa hayo ni magonjwa yanayosababishwa kwa kiasi kikubwa na utumiaji wa
kemikali katika vipodozi, ambapo athari zake huanza kuathiri mtoto akiwa bado
yuko tumboni.
Hospitali ya Mirembe hutoa
huduma za rufaa kwa wagonjwa wa magonjwa ya Akili. Katika mwaka 2004 iliweza
kutoa huduma ya wagonjwa wa nje 33,067
na waliolazwa 3,010. Idadi ya vifo
vilivyotokea katika mwaka 2004 kwa wagonjwa wa magonjwa ya akili ilikuwa
asilima 4.4 ya idadi ya wagonjwa
waliolazwa.
Magonjwa ya Akili kumi
yaliyoongoza kwa wagonjwa waliolazwa mwaka wa 2004 ni Schizophrenia 61%,
Epilepsy 229 (8.4)%, Organic brain syndrome 134 (6%), Acute psychosis,
Psychoactive substance use disorders 14% Depression, Alcoholic psychosis 2%
Manic-depressive psychosis, Mania 0.7%, Senile dementia 1.4%, Acute Psychosis
0.9%, Mental deficiency 0.5% na Anxiety neurosis 0.4%
Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI)
Taasisi ya
saratani ocean road ni taasisi maalum ya kutibu magonjwa ya Saratani, kwa mwaka
2004 ilihudumia wagonjwa wa nje (OPD) 6,962 ambapo wagonjwa 2,947 walikuwa wa
Saratani ya shingo ya uzazi na kati ya hao wagonjwa wapya walikuwa 992 na
waliokuwa wakifuatiliwa ni 1,955. Wagonjwa 4,015 walikuwa na Saratani za aina
nyingine ambapo 1,874 kati yao ni wapya na 2,141 walikuwa wakifuatiliwa.
Kuhusu
wagonjwa, wagonjwa 2,312 walilazwa mwaka 2004. Jumla ya vifo 187 vilitokea
kutokana na magonjwa ya Saratani. Saratani ya shingo ya uzazi iliongoza kwa
34.6% ikifuatiwa na Kaposis Sarcoma 14%, Oesophagial carcinoma 8.1 %, Saratani
ya matiti 8.0 % pamoja na Saratani za Head and Neck 7.8% kati ya magonjwa kumi
yaliyooongoza kwa magonjwa ya nje (OPD). Tiba ya mionzi ilitolewa kwa wagonjwa
30,045 ambapo Shingo ya uzazi ilioongoza katika viungo vilivyotibiwa kwa 65%,
ikifutiwa na Head and Neck 10.5% pamoja na Oesophagus 6.3%. Zingatia idadi
ya wagonjwa waliohudumiwa, waliokufa, jumla yao walioadhirika. Tazama pia
magonjwa yaliyowafanya wengi kulazwa katika taasisi hizo za Afya. Utagundua
kuwa vyanzo vya magonjwa hayo vinapatikana ndani ya vipodozi vinavyoonekana
kupendwa na kutumiwa na wanawake wengi. Je, watumiaji watapona kwa hali hii,
mabadiliko yasipofanyika?
Wapenzi watu wa
Mungu, hata katika nchi ya Tanzania, Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA), imepiga
marufuku baadhi ya vipodozi ambavyo vimeonekana kuwa na madhara makubwa kwa
binadamu. Ikiwa taasisi hii yaweza kuwa na kitu chema cha kuionya jamii
inayotumia vipodozi kumkosoa Mungu katika uumbaji wake, habari gani kwa sisi
watu wenye nuru ya Mungu?. Kwanini tusiridhike na jinsi Mungu alivyotuumba?
Huko ni kuwaka tamaa na kukosa kuwa na kiasi, ndipo tunafikiria kumkosoa Mungu
katika uumbaji wake. Wanawake wanajiwekea makalio yasiyo yao, kupunguza matiti
au kuyapandisha, kupaka rangi za kucha, mdomo na sehemu nyingine, kutumia dawa
za kuongeza hips, kutumia dawa za kukuza nywele, kuweka nywele za bandia na
kukoboa ngozi. Tusipo isikia sauti ya Mungu inayotuita leo kutoka Babeli,
tutaangamia kwa magonjwa yaliyotajwa hapo juu, ambayo chanzo chake kikubwa ni
matumizi ya hivyo vipodozi.
Soma taarifa ya
gazeti hili la Mwananchi hapo chini, iliyoripotiwa 24 May 2012 20:48
MWANANCHI:
Thursday,
24 May 2012 20:48
|
Daniel
Mjema, Moshi
WAKATI Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), ikipiga marufuku matumizi ya vipodozi hatari kwa afya za binadamu, vipodozi hivyo sasa vimetapakaa katika maduka mbalimbali ya vipodozi mkoani Kilimanjaro. Hali ni mbaya zaidi katika mji wa Moshi na vitongoji vyake ambapo baadhi ya Maofisa wa Afya wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, wamegeuza biashara hiyo kuwa mradi ambapo ‘humalizana’ kiaina na wamiliki wa maduka hayo. Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini baadhi ya maduka hayo kuuza vipodozi hivyo kwa usiri mkubwa kwa kutazama sura ya mteja ambapo sehemu kubwa ya wale wanaouziwa ni wanawake huku wanaume wakitiliwa mashaka. Vipodozi vilivyozagaa kwa wingi ni Carolight, Mekako, Maxi Light, Bio Carote, Carottene na G&G cream, Rico Cream, Princes Cream na Clare Cream ambavyo TFDA ilitangaza vipodozi hivyo kuwa na madhara makubwa kwa binadamu. Maduka yaliyosheheni vipodozi hivyo yapo katika stendi kuu ya mabasi Moshi Mjini, stendi ya Soweto, Barabara ya Nyerere maarufu kama Double Road, maeneo ya KCMC na baadhi ya maduka ya bidhaa za rejareja yaliyopo kwenye makazi ya watu. Katika kuthibitisha kuzagaa kwa vipodozi hivyo, mwandishi wa habari hizi aliamua kumkodi mwanamke mmoja na kuzunguka naye katika maduka sita kununua vipodozi hivyo na akauziwa japo vilikuwa vikichukuliwa nje ya makabati ya bidhaa. Habari zaidi zilidai kuwa Afisa mmoja wa Afya katika Manispaa ya Moshi(jina tunalo) amekuwa akipita katika maduka hayo mara moja au mbili kwa mwezi na kuchukua hongo ya kati ya sh100,000 na sh200,000 kwa kila duka. Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Dk. Christopher Mtamakaya alipoulizwa jana alisema hana taarifa juu ya kuzagaa kwa vipodozi hivyo na kuahidi kufanya operesheni ya kukagua maduka yote ya vipodozi. Tayari TFDA ilishatoa taarifa kwa umma juu ya kuwepo kwa vipodozi karibu 200 ambavyo vimetengenezwa kwa madini hatari ya Hydroquinine, Steroids, Bithionol na Zebaki ambayo yana madhara makubwa kwa binadamu. Taarifa hiyo ya TFDA inasema vipodozi hivyo hatari huweza kusababisha kansa ya ngozi kwa mtumiaji, akina mama kuzaa watoto wenye mtindio wa ubongo na uharibifu wa ini na figo na athari huchukua muda mrefu kutambuliwa. |
Historia
ya upambaji wa nywele katika Biblia.
Katika bibilia upambaji wa nywele
uliambatana na wanawake waovu, wauaji, Malaya na wenye mashetani au waabudu
mashetani. Kisa cha Yezebeli katika (2 Falme 9:30), kina onesha kuwa Yezebeli
alizaliwa katika Ikulu ya sidoni katika nyumba ya waabudu mashetani au miungu.
Miungu yao ilikuwa “ Baali au Bel” mungu mkuu wa kiume aliyeabudiwa
kwa kutoa kafara za wanadamu. Bibilia inashuhudia ibada ya namna hiyo. “Nao wamemjengea Baali mahali pake
palipo juu ili kuwachoma moto wana wao wawe sadaka za kuteketezwa kwa Baali
(yer 19:5)” kando ya ibada hiyo ya kuchoma watoto, ilijumuisha
uasharati.
Yezebeli akaolewa na Ahabu mfalme wa
Israel. Binti huyu hakuacha ibada ya Baali katika taifa la Israel (1falme
18:4). Hivyo wale wanaooa mabinti wanao jipamba wakidhani watawabadilisha
wanajidanganya huko ni kuleta moto wa kigeni katika familia yako na ndipo
mtaungana kuabudu miungu mingine.
Lakini Yezebeli alikuwa mwongo na
muuaji pia, (1 falme 21:1-16), ndipo baada ya miaka kadhaa, Yehu akaenda
kulipiza kisasi, akamkuta huyu mwanamke na tabia yake ya kupamba nywele,
Bibilia inasema “Yezebeli akapata
habari akatia wanja akapamba kichwa chake ………(2 falme 9: 30),
lengo lake la kufanya hivi kwanza aliamini miungu yake itamsaidia lakini pia
alitaka Yehu amtamani ili asimuue. Lakini Yehu alipomwona hakumhurumia alimuua
(2 Falme 9:33).
Kwahiyo tunaona kuwa upambaji wa nywele
si wa wanawake wa kristo. Bali kiasilia ni wa waabudu mashetani ambao huenda
sambamba na uovu, uuaji na uasherati. Kuweka nywele za badia zilizo na rasta,
kuweka rangi (nyekundu, nyeupe au kahawia na kadhalika) na kuweka wanja, hayo
yana kutia hasara kiuchumi, lakini pia yanaharibu sifa yako njema ya kiroho.
Ndugu wapenzi katika kristo nawasihi
kwa neema ya Yesu epukeni kupamba nywele maana hayo ni kwa waabudu mashetani.
Mungu anachotuagiza kufanya ni kutunza na wala sio kupamba nywele. “kujipamba
kwenu kusiwe kujipamba kwa nje, yaani kusuka nywele na kujitia dhahabu na
kuvalia mavazi(1peter.3:3).” kumbuka hapa maandiko yanazungumzia
kupamba si kutunza. Mapambo yanayo kubaliwa hapa na ndiyo yanayo zungumzwa ni
mapambo yasiyo haribika, yaani roho ya utulivu maana ndivyo walivyo jipamba
wanawake watakatifu wa zamani (1 pet.3:4).
Katika ufunuo 2:20 anatajwa mwanamke
kwa kuhusika na uovu kama uzinzi , “lakini nina neno juu yako ya
kwamba wamridhia Yule mwanamke Yezebeli yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha
watu wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa
sanamu”. pia mwanamke wa ufunuo 17 naye pia ameonekana amepambwa
lakini anatajwa kuwa mzinzi huwakilisha kanisa lililo asi.
Kwa hiyo ili nywele zako zikupatie
heshima na kuvutia kukubalika kwako zitunze katika hali ya usafi usiziache
zikakuletea usumbufu kichwani kama vile kuwasha na kuwa makao ya chawa na
uchafu. Kwa kuziweka nywele katika hali nzuri inakulazimu kuziosha vizuri mara
kwa mara kwa sabuni. Baada ya kuziosha zipake mafuta maalum ya nywele, sio
madawa. Usiache nywele zako zinasokotana na kufanya zisipendeze, na unapojaribu
kuzichana zinauma. Osha, paka mafuta na zichane. Biblia inasema “wala kichwa chako kisikose
marhamu (Muhubiri 9:8).” Kwa nini wewe unaacha nywele zako kuwa
chafu? Jaribu kutumia nywele zako kujipatia sifa njema, kanisani, nyumbani,
shuleni, chuoni, au katika jamii inayokuzunguka. Jiepushe na mitindo isiyompa
Mungu utukufu.
HITIMISHO:
MSIMAMO WA KANISA, THISDASO T.U, THISDASO DODOMA
ZONE.
1kor.4:1 – Mtu na atuhesabu hivi; kuwa tu watumishi wa
Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili,
ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.
Kwakweli kama wakristo, tunayo kila
sababu ya kuwa kielelezo katika maeneo tunayoishi ili kuwa nuru kwa watu
wengine wanaoteseka na mambo ya Dunia hii yasiyo na faida. “Na waende kwa
sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na Neno hili, bilishaka kwa hao
hakuna asubuhi” (Isaya 8:20). Kama wakristo ikiwa hatuendi sawasawa na Neno
sisi kwetu hakuna asubuhi, maana hatutakuwa nuru kwa wtu.
Watu wa Mungu huongozwa na Neno la
Mungu, ili liwakinge katika kushindana na mivuto ya walimu wadanganyifu na
nguvu za uongo wa pepo za giza. Shetani anatumia kila hila awezayo kuwazuia ili
awazuie watu kufahamu maarifa ya Biblia. Katika kila uamsho wa kazi ya Mungu,
mkuu wa uovu huamka kufanya bidii zaidi; anajitahidi kupita kiasi kushindana na
kristo na wafuasi wake. Angalia sana pepo hili baya la ibilisi la kutaka
kukwamisha kazi ya Mungu lisikutumie kwa kazi zake, tumwombe Mungu atupatie
uwezo wa kuzipinga hila za shetani, Tule kwa kiasi, Tunywe kwa kiasi, Tuhusiane
kwa kiasi, Tuvae kwa kiasi, Tuongee kwa kiasi huku tukijua kuwa sisi ni chumvi
ya Dunia.
Hii ni saa ya hatari kubwa.
Kitakacho vumilia mapigo saba ya mwisho
ni tabia iliyo takatifu. Hitaji muhimu……Hitaji kubwa la kanisa la masalio si
ongezeko la washiriki, wahubiri zaidi, au vifaa zaidi. Zaidi sasa hitaji kubwa
leo ni watu waume na wake waliojazwa na Roho Mtakatifu. Kumaliza kazi ya Mungu,
yatupasa tupokee kwa upya kila siku ubatizo wa Roho Mtakatifu.
“Hakuna hata mmoja anayedai utakatifu
ambaye ni mtakatifu wa kweli. Wale ambao wameandikwa kuwa ni watakatifu katika
vitabu vya Mbinguni hawajifahamu, nao huwa ni wa mwisho kujivunia wema wao
wenyewe”.
“Wale ambao kwa kweli wanatafuta
kukamilisha tabia zao za Kikristo hawatakubali kuwalazimu kuwa hawana dhambi.
Maisha yao yanaweza kuwa hayana hatia, wanaweza kuishi maisha yanayowakilisha
kweli walioipokea, kwa kadri wanavyoweka mawazo yao kudumu kwenye tabia ya
kristo, kwa kadri wanavyokaribia sura yake ya kimungu….”watakamilishwa nao
watayachukia mambo ya dunia hii yanayoonekana kuwavutia walio wengi.
Wale wanaojaribiwa kumsaidia Shetani
kulaumu viongozi na washiriki katika kanisa la masalio, watafanya vyema
kutafakari maonyo ya ujumbe wa Mungu katika mafungu yafuatayo; 6 T 42 – “Hhakuna chochote katika
ulimwengu huu kinachopendwa kama Kanisa la Mungu. Mungu ana kanisa ulimwenguni,
ambao ni watu wake waliochaguliwa wanaozishika amri zake. Anaongoza, si
machipukizi yanayofarakana, si mmoja hapa na pale, lakini watu waliopamoja”.
(kutayarisha njia sehemu ya pili, u.k 48).
“Hakuna kinacho mkosea Mungu kama tendo
la kudharau mvuto wa wale wanaoifanya kazi yake. Atawahesabia kosa wale wote
wanaomsaidia Shetani katika kazi yake ya kulaumu na kukatisha tama”
(kutayarisha njia sehemu ya pili, u.k 48). “Yatupasa tuwe na bidii kubwa.
Hatuna muda wa kutumia kwa kulaumu na kutoa mashitaka. (kutayarisha njia sehemu
ya pili, u.k 48). “Lolote lililo baya, la chuki, kulaumu, kudhulumu, hayo si ya
kristo, bali hutoka kwa Shetani” (kutayarisha njia sehemu ya pili uk 48)
“Kuvutwa kuingia katika kulaumu
wengine, kungekuwa ni ishara ya hatari kwetu, kwani roho mtakatifu
anapotutakasa na kutubadilisha, mioyo yetu itajazwa na upendo kwa ndugu zetu….”
“Ijapokuwa ni kweli kwamba wengi wetu katika kanisa la Masalio wako katika hali
ya Laodikia, ambao wengi watatikiswa na kutolewa, hata hivyo kanisa wako walio
waaminifu ambao watasikia mashauri ya Kristo aliye Shahidi wa
kweli…watatayarishwa kwa mvua ya masika, wakishiriki katika kutoa ujumbe pamoja
na Kilio Kikuu na kuwa tayari kubadilishwa.
“Hili ni kanisa la Masalio. Mungu hataongoza
kanisa lingine. Sasa ni wakati wa kujitayarisha kwa mvua ya masika. Na
tungekumbuka kila siku kuwa kazi hii ya kujitayarisha yapasa ianze wakati wa
mvua ya vuli” (kutayarisha njia sehemu ya pili uk 48)
Furaha yetu ya baadaye inategemea kuwa
ubinadamu wetu, na uwezo wake wote, view katika kumtii Mungu na kuweka chini ya
utawala wa Kimungu…” “Kristo anatamani kuwa kila mmoja wetu akate shauri
mapema” “Bidii isiyo na kikomo ingekuwa yetu sasa”
Mwisho.
“Ombeni kuwa nguvu ya Roho Mtakatifu,
ikiwa na uwezo wake mwenyezi, unaohuisha na kugeuza, uijie roho iliyolemaa kama
nguvu ya umeme ikiufanya kila mshipa kuamka kwa uzima mpya, kumhuisha mwanadamu
kutoka kwa ufu wake wa kidunia na hali ya kimwili”.
Mungu awabariki mnapojiandaa kila mmoja
wetu kufanya mabadiliko kwa yale ambayo Roho amekushuhudia kupitia somo hili ya
kwamba ufanye matengenezo.
BWANA
AWABARIKI.
Somo hili
imeandaliwa na mainjiristi wafuatao;
-CHERLES ANTHONY. (MSAIDIZI M/KIROHO THISDASO DODOMA ZONE).
-MOGENGE EMMANUE S. (MKUU M/KIROHO - THISDASO DODOMA ZONE).
-GIDION HABILI.
(M/KITI – THISDASO DODOMA ZONE).
- KESHI MARTIN
MALEHIWA. (M/KITI - THISDASO TANZANIA UNION).
VIELELEZO VYA NUKUU
CD - Counsels or Diet and Foods.
Te - Temperance.
T - Testimonies for the
church Volume I
MH - The Ministry of Healing
PP - Patriarchs and Prophets
CS - Counsels on Stewardship
Ed - Education.
-Nusuru Ndoa yako. By
Pr.Makoye
-Kuchagua
Mchumba. By E.G White
-kutayarisha
njia sehemu ya pili.
Limeandaliwa na Emmanuel Mogenge THISDASO DODOMA ZONE.
No comments:
Post a Comment